Synopsis
Kupitia vipindi vyetu tunajaribu kuwahamasisha vijana wa Afrika kuhusu elimu ya jamii. Inasaidia kuyafanya maisha yao kuwa rahisi.
Episodes
-
Ardhi ya Ahadi – Hadithi ya Uhamiaji wa Waafrika barani Ulaya
12/08/2013 Duration: 11minHuku Farahani na Sule wakiota kuwa na maisha bora Ulaya, mwanafunzi Linda tayari yuko njiani kuelekea huko. Mchezo huu unalinganisha ndoto za vijana wa Kiafrika za kusoma na kufanya kazi Ulaya na hali halisi ya mambo.
-
Haki za binaadamu ni za watu wote lakini...
06/08/2013 Duration: 12minKila binaadamu hapa duniani ana haki ya uhuru na usawa - kwa mujibu wa azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binaadamu. Lakini katika mataifa mengi barani Afrika, utakuta haki hizi zinaendelea kukanyagwa na kukiukwa.
-
Kazi –Kipindi 8 – Mwanamuziki
16/03/2011 Duration: 10minKatika kipindi hiki, tutageuka na kuangazia sekta ya muziki na kupata nafasi ya kumfahamu Chimere Emejuobi, mwimbaji kutoka Lagos. Muziki ni muhimu sana katika jamii nchini Nigeria.
-
Kazi – Kipindi 7 – Vijana wasio na ajira
16/03/2011 Duration: 10minHatutazungumzia juu ya taaluma fulani, lakini ni juu ya wale wote ambao hawana ajira. Idadi ya wasio na ajira hususan miongoni mwa vijana imeongezeka sana barani Afrika. Kila kijana mmoja kati ya watano hana ajira.
-
Kazi – Kipindi 6 – Kazi za sekta isiyorasmi
16/03/2011 Duration: 10minKatika mji mkuu wa Kenya, tunakutana na watu wanaofanya shughuli zao ambazo ziko nje ya sekta rasmi ya uchumi. Wanashughulika kinyume na sheria bila ya kuwa na elimu stahiki, mfano biashara ya kiwango cha rejareja.
-
Kazi – Kipindi 5 – Mwalimu
16/03/2011 Duration: 10minTutaiangazia sekta ya elimu huko Lagos Nigeria. Kwa jumla waalimu hulipwa mshahara mdogo. Lakini kwa baadhi yao, la muhimu ni hamasa ya kufundisha na hamu ya kuwapatia ufahamu wanafunzi wao.
-
Kazi – Kipindi 4 – Meneja wa Hoteli
16/03/2011 Duration: 10minKatika kipindi hiki tutapata nafasi ya kumfahamu kijana mmoja nchini Uganda ambaye ni meneja wa hoteli. Je kuna ugumu gani wa kufanya kazi ya umeneja wa hoteli katika nchi zinazoendelea kama Uganda?
-
Kazi – Kipindi 3 –Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari
16/03/2011 Duration: 10minMtandao wa Intaneti ni lango kuu la kujiunga na jamii duniani. Hata hivyo bado watu wengi hawana uwezo wa kuitumia. Wafanyakazi katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wanajaribu kulibadilisha suala hili.
-
Kazi –Kipindi 2 – Fundi magari
16/03/2011 Duration: 10minKuna taaluma ambazo zinachukuliwa kuwa ni za wanaume tu. Ni wanawake wangapi wanaoweza kurekebisha magari au pikipiki? Estelle Christian Ouedraogo, kutoka Burkina Faso, ni miongoni mwao. Tujiunge naye!
-
Kazi – Kipindi 1 – Nesi
16/03/2011 Duration: 09minKatika mfulululizo huu, tutakutambulisha kwa vijana wa kiafrika wenye taaluma mbalimbali, na kukupatia undani wa shughuli zao. Kwanza tutapata nafasi ya kumfahamu Judith ambaye ni nesi katika hospitali huko nchini Kenya.
-
Ngano za Afrika – Kipindi 10 – Tumbiri na Kobe
16/03/2011 Duration: 11min“Wanaopata, wanaoweka. Anayepata kitu fulani njiani anaruhusiwa kukimiliki” Je, ni rahisi namna hiyo kila mara? Sikiliza hadithi ya kobe na tumbiri mjanja aliyelazimika kupata adhabu kuokoa mkia wake!
-
Ngano za Afrika – Kipindi 09 – Mrembo kuliko wote
16/03/2011 Duration: 10minHadithi yetu inatokea zamani za kale, wakati tausi alipokuwa angali mweupe. Jifunze jinsi alivyopata rangi zake nyingi na wakati huo huo kuiharibu sauti yake
-
Ngano za Afrika – Kipindi 08 – Bundi na Nyenje
16/03/2011 Duration: 12minSiku moja bundi mzee na nyenje kijana wanakuwa majirani. Mwanzoni wanafurahia kuishi kwa pamoja, lakini kadri muda unavyopita bundi anakasirika na nyenje anavunjika moyo. Watafanya nini?
-
Ngano za Afrika – Kipindi 07 – Dikum Dakum
16/03/2011 Duration: 12minKatika hadithi hii, marafiki zetu wanyama wenye njaa wanalazimika kutafuta njia ya kuchuma matunda mtini. Inaonekana kuwa kazi rahisi lakini mti wa maajabu wa marula unawafunza somo zuri
-
Ngano za Afrika – Kipindi 06 – Mfalme asiye na Ufalme
16/03/2011 Duration: 12minMwanamke kizee akamwambia Amadou. “Usijiingize katika hali usizoweza kukabiliana nazo! Fuata maagizo yangu.” Lakini wakati mwingine inahitaji uhodari mkubwa mtu kukubali udhaifu wake, kama Amadou atakavyogundua
-
Ngano za Afrika – Kipindi 05 – Kassi na Kaloo
16/03/2011 Duration: 10minKassi na Kaloo – marafiki wasioweza kutenganishwa! Angalau hali ilikuwa hivyo kabla farasi hao wawili wa kupendeza kupandwa na wafalme wawili mahasimu. Watafanya nini wakati vita vitakapozuka kati ya falme zinazopigana?
-
Ngano za Afrika – Kipindi 04 – Fisi, Nyoka, Chui na Ngiri
16/03/2011 Duration: 11minJe unaamini hirizi za bahati na mawe ya mazingaombwe? Sawa, zuia wazo hilo na tumruhusu ngiri atueleze hadithi yake kuhusu kilichomuokoa, na vipi
-
Ngano za Afrika – Kipindi 03 – Lipua Lipua
16/03/2011 Duration: 12minFuata nyayo za Lipua! Njiwa jasiri ana kibarua cha umuhimu mkubwa. Je Lipua atamshinda mfalme mlafi na muovu Karamba na kuwaokoa ndege wenzake wasife kutokana na njaa?
-
Ngano za Afrika – Kipindi 02 – Simba, Fisi na Tai
16/03/2011 Duration: 09minZamani paliondokea simba na fisi mwenye njaa. Kilichoanza kama uhusiano wa ajabu lakini wa furaha, kinamalizika huku fisi akiwa amejeruhiwa maisha yake yote na tai akipoteza manyoya yake kadhaa
-
Ngano za Afrika – Kipindi 01 – Masaibu ya Chura Mbott
16/03/2011 Duration: 12minKatika mfululizo mwingine wa kusisimua, tunautembelea ulimwengu wa mjusi kafiri Sindakh na chura aitwaye Mbott – hadithi kuhusu urafiki, uaminifu na usaliti