Synopsis
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.
Episodes
-
Zumbukuku nyimbo za taarab zinazokumbukwa hata sasa
03/08/2024 Duration: 20minZumbukuku ni miongoni mwa nyimbo zilizofanya vizuri katika muziki wa taarab, hii inashehenezwa na sauti ya kipekee ya kiume inayosikika katika muziki huo, Ally Star ndie aliyeimba wimbo huo; Ungana na Steven Mumbi katika makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Ally Star kuhusu namna nyimbo hizo zilivyotia fora.
-
Mwanamuziki Ogisha Matale atoa wito wa amani mashariki mwa DRC
27/07/2024 Duration: 20minMakala ya nyumba ya sanaa wiki hii imepiga kambi mjini Goma huko mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambako mwanzoni mwa mwezi mei mwandishi wetu Ruben Lukumbuka alikutana na msanii Ogisha Matale ambapo katika shughuli zake zake amekuwa akijaribu kuhimiza amani nchini, hususan eneo lake lenye kushuhudia mapigano ya mara kwa mara.
-
Mwanamziki Nyota Tiger mwalikwa wa makala Nyumba ya sanaa
20/07/2024 Duration: 20minNyota Tiger ni mzaliwa wa jijini Mwanza nchini Tanzania alilazimika kusafiri mpaka maeneo ya kusini mwa Afrika kukwepa adha za wazazi kumnyima fursa ya kufanya muziki. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.
-
Mchango wa sanaa ya muziki wa asili katika usuluhishi wa mizozo DRC
13/07/2024 Duration: 20minKatika makala ya nyumba ya sanaa wiki hii mwandishi wetu Ruben Lukumbuka ambaye hivi karibuni alitembelea mashariki mwa DRC ambako alikutana na Olivier wabahavu, msanii maarufu sana kufuatia nyimbo zake anazoimba katika lugha ya kihavu na kishi huko Kivu kusini na kaskazini, amezungumzia mchango wa sanaa ya muziki wa kiasili katika usuluhishi wa migogoro ya kivita mashariki mwa DR Congo.