Synopsis
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.
Episodes
-
Mchakato wa kuondolewa madarakani naibu rais wa Kenya, mazishi ya waliokufa Goma
12/10/2024 Duration: 20minWabunge 281 walipiga kura ya ndio kumwondoa naibu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua madarakani, mazishi ya watu waliokufamaji katika ajali ya Meli huko Goma DRC, ziara ya mkurugenzi wa kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa barani Afrika, Dr Jean Kaseya, nchini Rwanda kutathmini mikakati ya kupambana na mlipuko wa MPOX pamoja na marburg, mafuriko makubwa nchini Mali, mashambulio ya jeshi la Israeli dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon, mchakato wa uchaguzi mkuu kule Marekani. Ungana na Ruben Lukumbuka kusikiliza zaidi
-
Mswada wa kumwondoa naibu rais wa Kenya Kachagua, watu zaidi 78 wafamaji DRC
05/10/2024 Duration: 20minMakala imeangazia mchakato wa kumwondoa madarakani naibu wa rais wa Kenya Rigathi Gachagua, makumi ya watu wafamaji katika ajali ya boti huko Goma mashariki mwa DRC, hali nchini Rwanda na ugonjwa wa murburg, Uganda na Sudan, siasa za Nigeria na maeneo mengine ya Afrika magharibi, mashambulio ya jeshi la Israeli dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon na yale ya Hezbollah nchini Israeli na mambo mengine.
-
Lisu kuishitaki Tanzania kwa jaribio la kumuua, Kenya kupeleka polisi Haiti
28/09/2024 Duration: 20minMwanasiasa wa upinzani kule Tanzania Tundu Lisu kuishitaki serikali na kampuni ya mawasiliano TIGO kwa jaribio la kumuua, rais wa Kenya William Ruto alisema polisi 2500 watapelekwa Haiti, wakati rais wa DRC Félix Tshisekedi atoa wito kwa jumuia ya kimataifa kuiwekea vikwazo Rwanda kwa kuivamia nchi yake na kushirikiana na waasi wa M23, hali nchini Sudan, siasa za Senegal na maeneo mengine ya Afrika magharibi, mashambulio ya jeshi la Israeli dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon na mengineyo.
-
Rais wa Tanzania Samia Suluhu na wanadiplomasia, msamaha kwa mkuu wa polisi Kenya
21/09/2024 Duration: 20minMakala hii imeangazia kauli ya rais wa Tanzania kwa mabalozi wanaowakilisha nchi zao ilivyozua gumzo katika uga wa kimataifa, msamaha wa mahakama kwa afisa mkuu wa polisi Kenya, ziara ya mjumbe wake katibu mkuu wa umoja wa mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu ulinzi wa amani Jean Pierre Lacroix huko DRC, UN kughadhabishwa na kuahirishwa uchaguzi wa sudan Kusini, jeshi Ia Israeli lashambulia Hezbollah kwa kulipua vifaa vyao vya mawasiliano na kwengineko duniani.