Wimbi La Siasa

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 4:02:42
  • More information

Informações:

Synopsis

Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa

Episodes

  • Kenya: Upinzani utamtikisa Ruto uchaguzi wa mwaka 2027 ?

    30/04/2025 Duration: 10min

    Wanasiasa wakuu wa upinzani nchini Kenya, wakiongozwa na aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua, Aprili 29 2025, walikutana jijini Nairobi kuanza mikakati ya kuunda muungano mpya, kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Je, muungano huu ambao pia umemjumuisha aliyekuwa Waziri wa usalama Fred Matiang’i, unaweza kumtikisa rais William Ruto  wakati wa uchaguzi huo ?

  • DRC: Kabila aripotiwa kufikia Goma, huku chama chake kikifungiwa

    23/04/2025 Duration: 10min

    Rais wa zamani wa DRC, Joseph Kabila, Aprili 18, aliripotiwa kurejea nchini na kufikia jijini Goma, linalodhibitiwa na waasi wa M 23. Hata hivyo, taarifa hizi hazijathibitishwa rasmi. Serikali jijini Kinshasa, nayo imesitisha shughuli zote za kisiasa za chama chake cha PPRD. Kabila anashtumiwa na serikali kwa kuunga vitendo vya waasi hao.

  • Tundu Lisssu afunguliwa kesi ya uhaini, CHADEMA matatani

    16/04/2025 Duration: 09min

    Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani  nchini Tanzania, CHADEMA, Tundu Lissu, Aprili 10 alifunguliwa kesi ya uhaini, baada ya kukamatwa akiwa kwenye kampeni ya kisiasa, kushinikiza mageuzi kwenye mchakato wa uchaguzi, uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba.

  • Tanzania: CHADEMA yashinikiza mabadiliko kabla ya Uchaguzi Mkuu

    09/04/2025 Duration: 09min

    Mwezi Oktoba 2025, wananchi wa Tanzania, watashiriki kwenye uchaguzi Mkuu, kuwachagua madiwani, wabunge na rais. Hata hivyo, chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA, kikiongozwa na Mwenyekiti wake, Tundu Lissu, kinashinikiza mageuzi kwenye sheria za uchaguzi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo.Je, kitafanikiwa katika harakati zake ?

page 2 from 2