Synopsis
Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.
Episodes
-
DRC : Mchango wa AU kumaliza mizozo Africa
16/12/2024 Duration: 10minMoses Balagisi, afisi kutoka shirika la umoja wa Africa linaloshirikiana na masharika ya kiraia, kuhakikisha uongozi wa juu wa AU unaskiza kilio cha raia wa chini, analeza namna gani wanahakikisha hilo linafanyika. Kufahamu mengi zaidi, skiza makala haya.
-
Kenya :Madaktari watishia kugoma tena tarehe 22 Disemba
09/12/2024 Duration: 10minWahudumu wa afya nchini Kenya wanaitaka serikali kuwatuma kazini wanafunzi na wahudumu wa afya mara moja na kufuta malimbikizo ya mishahara ya madaktari kulingana na Makubaliano ya Pamoja ya 2017. Wahudumu wa afya ambao wamehudumu kwa miaka minne chini ya kandarasi katika taasisi za afya ya umma wanadai ajira ya kudumu ambayo walikuwa wamehakikishiwa na serikali ya Kenya kufuatia miaka mitatu ya huduma.
-
DRC : Haki ya mtoto kupata elimu na vizingiti vinavyochangia
12/11/2024 Duration: 10minKatika makala haya tunajadili haki za mtoto kupata elimu nchini DRC, hapa mkuu wa chuo cha walumu cha ISP, Butua Balingane anafafanua vizingiti vya mtoto kupata elumu nchini DRC. Kufahamu mengi skiza makala haya.