Synopsis
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .
Episodes
-
Ushirikiano wa kibiashara kati ya Kenya na Ufaransa
19/03/2025 Duration: 10minMsikilizaji juma moja lililopita, mtandao wa wafanyabishara na makampuni ya Ufaransa hapa nchini Kenya, walikutana na wenzao wa Kenya kuangalia namna bora zaidi ya kushirikiana hasa katika masuala ya teknolojia. Kwa mujibu wa takwimu zilizoko hali ya biashara za mtandaoni kikanda inaendelea kuimarika, huku matarajio ya matumizi ya akili mnemba yakionekana kuleta mageuzi makubwa katika sekta hiyo. Victor Moturi alizungumza na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia wa Kenya, William Kabogo.
-
Miundombinu; changamoto ya upatikanaji wa nishati (umeme) Afrika
12/03/2025 Duration: 10minWiki hii katika makala ya Gurudumu la Uchumi, tunajadili changamoto za upatikanaji wa nishati ya uhakika barani Afrika, ambapo pamoja na baadhi ya mataifa kuwa na rasilimali za kutosha kuzalisha nishati ya ziada, suala la miundombinu limeendelea kusalia kikwazo, ambapo baadhi ya mataifa yanalazimika kununua nishati toka mataifa jirani.Ali Mkimo, mchambuzi na mtaalamu wa masuala ya Uchumi atakuwa nasi kudadavua hili kwa kina.
-
Athari kwa uchumi wa dunia kutokana na vikwazo vya kibiashara vilivyotangazwa na Marekani
05/03/2025 Duration: 09minKatika makala ya Gurudumu la Uchumi juma tunajadili athari za kibiashara kimataifa kutokana na hatua ya hivi karibuni ya Marekani kutangaza vikwazo vya kikodi kwa mataifa ya Canada, Mexico, India na Uchina ambao ni washirika wake wakubwa kibiashara.Kujadili hili, kwenye line ya simu tunaungana na Profesa Wetengere Kitojo, mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.
-
Sehemu ya Pili: Afrika na harakati za kudai mabadiliko kwenye taasisi za kifedha za kimataifa
26/02/2025 Duration: 09minMsikilizaji juma lililopita tulianza kwa kujadili yaliyotokana na mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika, na suala kuu lilikuwa ni je, nchi za Afrika zitafanikiwa kushinikiza mabadiliko katika taasisi za kifedha za kimataifa na kuondokana na mikopo na madeni yasiyostahimilika ?Leo katika makala ya Gurudumu la Uchumi, nakuletea sehemu ya pili ya mjadala huu, nimemualika Ali Mkimo, mtaalamu namchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa nchini Tanzania.