Changu Chako, Chako Changu

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 7:50:19
  • More information

Informações:

Synopsis

Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.

Episodes

  • Historia ya Kenya kupata Uhuru pamoja na Maonyesho ya Sanaa ya Uchoraji Alliance Francaise Nairobi

    15/12/2024 Duration: 19min

    Makala haya yataangazia Historia ya nchi ya Kenya na jinsi ilivyopata Uhuru,kwenye kipengele cha pili utaskia safari ya vijana wanaofanya sanaa ya Uchoraji kutoka shirika lisilo la kiserikali la Uweza Art Gallery na mwisho kabisa kwenye kipengele cha historia ya mwanamuziki utaskia historia yake Juma Jux kutokea Tanzania.

  • Teknolojia yabadilisha muziki ,Ujio wake Msanii Sean Paul nchini Kenya

    08/12/2024 Duration: 19min

    Tutaangazia historia ya muziki wa Afrika, tukiangalia mabadiliko makubwa yaliyotokea kabla na baada ya kuibuka kwa teknolojia. Muziki wa Afrika ni sehemu muhimu ya utamaduni wetu, na umetumika kwa karne nyingi kama njia ya kuwasiliana, kusherehekea, na kuponya.

  • Hatuwa za mwisho za maandalizi ya tamasha la watu wa kabila la bashi la desemba 6

    01/12/2024 Duration: 20min

    Uhusiano baina ya lugha na utamaduni, mila na mirathi ya jamii kwa jumla huenda ukafahamika angalau kwa wepesi, iwapo tutazingatia mambo kadhaa ikiwemo lugha na matumizi yake, tabia, utu, utamaduni, mila,mitindo na mengineo. Watu wa kabila la washi mashariki mwa DRC wameandaa tamasha la kutambulisha utamaduni wao, ambalo ni msimu wa pili na limepangwa kufanyika desemba 6 hadi 8 huko Bukavu. Katika makala haya mtangazaji wako Ali Bilali anakuletea sehemu hii ya tatu na ya mwisho ya maandilizi ya makala haya. unaweza kusikiliza sehemu ya kwanza kubonyeza hapa (sehemu ya kwanza) Lakini pia sehemu ya pili kwa kubonyeza hapa (Sehemu ya pili) Asante kwa kuendelea kuwa muaminifu kwa radio yako na kwa mtangazaji wako asiependa makuu unaweza kumfollow kwa kubonyeza hapa Billy Bilali

page 2 from 2