Synopsis
Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.
Episodes
-
Mafundisho potofu kutoka kwa baadhi ya viongozi wa dini Afrika Mashariki
16/05/2024 Duration: 09minTunaangazia namna viongozi wa dini wamekuwa kinara katika kupambana na mafundisho potofu na kutumia mahangaiko ya waumini wao kama mtaji wa kuvuna utajiri.
-
Juhudi za kupambana na ulawiti wa watoto katika nchi za Afrika mashariki
09/05/2024 Duration: 09minUlawiti ni janga linaloendelea kuwakumba watoto si tu katika mataifa ya ukanda wa Afrika mashariki bali katika mataifa mbalimbali ulimwenguni. Nchini Tanzania kumekuwa na takwimu za kupanda na kushuka huku baadhi ya wanaharkati wakisema kuwa swala la uzembe limekuwa likichangia kuongezeka kwa ubakaji na ulawiti kwa WatotoHatua mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa na kuibua wito wa kitaifa kwa wazazi kuongeza ulinzi na ufuatiliaji wa watoto wao.
-
Ujumbe unaoandikwa kwenye vyombo vya usafiri katika mataifa ya Afrika
01/05/2024 Duration: 09minJe ujumbe unaoandikwa unahalisia na vitu vilivyowatokea makonda na madereva wa vyombo hivyo.
-
Tanzania:Juhudi za wabunifu katika kupunguza hewa ya ukaa kutunza mazingira
18/04/2024 Duration: 09minSerikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Masuala na Utalii, katika taarifa ya misitu na ufugaji nyuki inabainisha kuwa mkaa ni chanzo kikubwa cha nishati ya kaya katika maeneo ya mijini kwa kupikia na kupasha joto, kwa kuwa inachukuliwa kuwa ya bei nafuu na inapatikanakwaurahisi. Inakadiriwa kuwa asilimia 85 ya watu wote wa Tanzania kutegemea nishati ya majani. Nishati ya kupikia ndiyo inayoongoza kwa matumizi ya biomasi katika kaya ikilinganishwa na sekta nyingine kama vile ujenzi na kilimo sekta ya msingi.