Habari Za Un

Dkt. Tedros: Heshima kwa wahudumu wa afya wa Rwanda wanavyopambana na Marburg

Informações:

Synopsis

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani amewapongeza wahudumu wa afya wa nchini Rwanda kwa kazi kubwa wanaoyoifanya kukabiliana na ugonjwa wa Marburg. Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameeleza hisia zake hizo mwishoni mwa wiki alipofanya ziara katika vituo mbalimbali vya afya katika mji Mkuu wa nchi hiyo, Kigali."Ninawapongeza wahudumu wa afya waliojitolea ambao wamejiweka hatarini kuokoa wenzao, na ambao wameendelea kufanya kazi licha ya hatari. Na ninaenzi wale ambao tumewapoteza."Pia Dkt. Tedros akaeleza kuwa yeye na wenzake wamefurahishwa na namna ya utoaji huduma ambayo haijawahi kutumiwa katika mlipuko ya magonjwa ya namna hii barani Afrika akitolea mfano wagonjwa wawili aliowashuhudia wakiendelea vizuri kwamba waliokolewa kwa kuwekewa mipira iliyopeleka hewa ndani ya mwili.“Tunaamini hii ni mara ya kwanza kwa wagonjwa wenye virusi vya Marburg barani Afrika kuingiziwa na kutolewa mpira wa hewa. Wagonjwa hawa wangefariki dunia katika milipuko ya hapo awali. Hii inaonesha kazi a