Habari Za Un

COP16: Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Baionuai waanza nchini Colombia

Informações:

Synopsis

Mkutano wa 16 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa bayonuai (COP16) umeng’oa nanga leo katika mji wa Santiago de Cali au Cali huko nchini Colombia ambapo mataifa 196 yatajadili jinsi ya kusitisha na kubadili mwelekeo wa kudorora kwa ulimwengu wa asili. COP16  kwa siku 12, viongozi na wadau kutoka kote duniani wanatarajiwa kujadili  namna ya wanadamu kuishi kwa amani na asili ya ulimwengu, kama wasemavyo nchi  mwenyeji Colombia kwa lugha ya kihispanyola Paz con la Naturaleza yaani amani na asili.Washiriki, kwa kina watajadili utekelezaji wa mkakati wa Kimataifa wa Kunming-Montreal kuhusu bayoanuai, makubaliano ya kihistoria ya mwaka 2022 ya kusitisha na kubadili upotevu wa asili. Pia watachunguza jinsi ya kuelekeza mabilioni ya dola kwa nchi zinazoendelea ili kuhifadhi na kudhibiti bioanuai kwa uendelevu. Na watajadili sheria za msingi ambazo zinaweza kuhitaji kampuni za kibinafsi kufidia mataifa.Katika sherehe za ufunguzi wa mkutano huu hapo jana, kwa njia ya video, Katibu Mkuu wa