Synopsis
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
Episodes
-
Maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani
09/12/2024 Duration: 09minKatika makala haya, tutazungumza na watu muhimu kama vile mgonjwa wa UKIMWI, daktari, na mkunga anayeelimisha kuhusu jinsi ya kuzuia watoto kuambukizwa virusi vya UKIMWI wakati wanapozaliwa. Pamoja, tutafahamu changamoto, mafanikio na hatua zinazochukuliwa katika vita hivi.
-
Dunia: Wahudumu wa afya waendelea kuuawa katika maeneo ya mizozo
07/12/2024 Duration: 10minUmoja wa mataifa umeorodhesha mwaka 2024 kama mwaka hatari zaidi kwa wafanyikazi wa mashirika ya kimsaada Katika takwimu za UN ,wafanyakazi zaidi ya 200 wamewauwa katika mzoz wa Gaza na wengine zaidi ya 20 katika mzozo wa Sudan
-
Afya ya kujifungua na uzazi: Changamoto zinazotokea wakati wa kujifungua mtoto
12/11/2024 Duration: 10minIdadi kubwa ya kina dada wameamua kuchagua upasuaji kama njia rahisi ya kujifungua kwa sababu tofauti tofauti.Sehemu ya pili ya makala haya inaangazia ni kwa nini idadi hio inaongezeka kisha hali inakuaje pale kwenye chumba cha kujifungulia.Dakatari Lilian Nkirote kutokea hospitali ya Jacaranda jiji Nairobi anaelezea kwa kina.
-
Afya ya uzazi na kujifungua
08/11/2024 Duration: 10minMakala ya siha njema wiki hii tunaangazia Afya ya uzazi na kujifungua na sio safari nyepesi.Ni safari yenye changamoto haba na furaha kwa wanawake na familia zao. Ni muhimu kwa kila mama mjamzito kufahamu hatua muhimu za kuhakikisha ustawi wa afya yake na ya mtoto anayemtarajia. Kupitia huduma bora za kiafya na ushauri wa wataalamu, wanawake wanaweza kufurahia safari ya uzazi kwa usalama na utulivu.