Siha Njema

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 3:58:16
  • More information

Informações:

Synopsis

Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.

Episodes

  • Kliniki tembezi za figo zinavyowasaidia wagonjwa wa figo nchini Kenya

    07/04/2026 Duration: 10min

    Idadi ya wagonjwa wa figo imekuwa ikiongezeka kutokana na kuongezeka pia kwa magonjwa yasiyoambukiza kama vile Kisukari.

  • Magonjwa ya Autoimune yana uwezo kukusababishia magonjwa mengine zaidi

    31/03/2026 Duration: 10min

    Magonjwa yanayoshambulia kinga yanapompata mtu ,huendelea kusambaa ,kudhuru kingamwili na  kumweka hatarini mgonjwa kiasi cha kuwa mgonjwa anaweza kupatwa na magonjwa zaidi ya moja ya aina hiyo. Elwyn Chebet aligunduliwa na Lupus na baadaye akajikuta anapambana na magonjwa zaidi ya tano aina ya Autoimmune. Mwezi Machi ambapo ulimwengu huelekeza kurunzi kwenye magonjwa ya mfumo wa kinga au Autoimmune,watalaam wanasikitika kuhusu ufahamu mdogo kuhusu magonjwa haya. Wagonjwa wengi huwa na dalili za kukanganya na ubainishaji wa magonjwa haya unaweza kuchukua muda mrefu na kugharimu kiasi kikubwa cha pesa. Na kwa kuwa vyanzo vya magonjwa haya huwa haviko wazi matibabu yake huwa yenye mtihani mkubwa.Watalaam wengi hujaribu kutibu dalili bila kushughulikia chanzo cha ugonjwa wenyewe. Katika makala haya tumezungumza na Elwyn Chebet ambaye ni shujaa na mwanaharakati wa ugonjwa wa Lupus ambao huathiri viungo kadhaa mwilini na hata ngozi. Katika simulizi yake ,anaeleza kuwa kutokana na kinga dhaifu magonjwa tegemezi ka

  • Visa vingi vya TB Afrika bado vinapatikana miongoni mwa vijana hasa wanaume

    24/03/2026 Duration: 10min

    Watalaam wanasema vijana wengi hufikia kwenye maduka ya kuuza dawa kupata huduma za afya baadala ya kufika hospitali kufanyiwa vipimo Unyanyapaa pia inachangia wanaume au vijana kuwa na ari ya kwenda kupata huduma za afya haswa za TB.

  • Nini magonjwa yanayoathiri kinga mwili au Autoimmune

    24/03/2026 Duration: 10min

    Unapopata magonjwa ambayo yanaathiri kinga ya mwili wako,ina maana kuwa kinga yako inaweka mifumo yote ya mwili kwenye hatari. Unaweza kujikuta unapata magonjwa kama Lupus,ugonjwa wa Tezi Koo au Mifupo yako kuwa nyepesi kiasi cha kuvunjika kwa urahisi. Ubainishaji wa magonjwa haya unahitaji subira na ufuatialiaji wa karibu ili kuelewa kila dalili anayoonesha mgonjwa .Gharama yake basi inamanisha ni ya juu na huhitaji muda mrefu.

  • Kampeni ya kumaliza unyanyapaa wa siku za hedhi kwa kushirikisha wanaume

    20/03/2026 Duration: 10min

    Siku za hedhi huchukuliwa kuwa swala la wanawake na halifai kuzungumzwa hadharani kwa jamii nyingi .Hali hii imesababisha wanawake na wasichana kupitia unyanyapaa ijapokuwa hili ni swala la haki ya uzazi

  • Madhara ya afya ya akili yanayotokana na matumizi ya kupitiliza ya simu

    03/03/2026 Duration: 10min

    Ripoti ya afya akili  duniani ,inaonya kuhusu madhara yanayotokana na matumizi ya simu za mkononi miongoni mwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 na 34 Katika mataifa ya Afrika ambapo matumizi ya simu hizi huanza kwa kuchelewa ,vijana walionekana kuwa afadhali ikilinganishwa na mataifa kama Finland ambapo watoto huanza kutumia simu katika umri mdogo mno.   Katika mataifa yaliyozingatia maswala ya dini na muunganiko wa familia na jamii walionekana pia kuwa na ahueni.

  • Fahamu madhara ya mvua kubwa kwa afya yako na namna ya kujikinga

    24/02/2026 Duration: 08min

    Mvua kubwa inaendelea kunyesha katika mataifa mengi ya Afrika ikisababisha mafuriko makubwa ,maafa na uharibifu wa mali Mvua ingawaje ni baraka, kunaponyesha ghafla inaweza kuwa chanzo cha baadhi ya magonjwa kama vile Malaria, Kipindu Pindu na magonjwa ya kusambazwa na minyoo.

  • Kupambana na ugonjwa wa mbwa kichaa Nairobi kwa kuzingatia maslahi ya mbwa

    10/02/2026 Duration: 10min

    Mamlaka jijini Nairobi zimefanya operesheni kudhibiti ongezeko la mbwa mtaa katika mkakati wa kupambana na ugonjwa wa mbwa kichaa Mbwa japo anasemekana kuwa rafiki wa karibu na mwaminifu unapomfuga ,matunzo yasiyofaa au kuwatelekeza unaweza kukuweka karibu na ugonjwa wa mbwa kichaa Ukiwa utamfuga mbwa ,sharti kuzingatia usafi na chanjo ya kila mwaka dhidi ya ugonjwa wa mbwa kichaa

  • Kwa nini kuna umuhimu wa kutumia dawa za minyoo baada ya miezi sita

    05/02/2026 Duration: 09min

     Shirika la afya duniani ,WHO hupendekeza matumizi ya dawa za minyoo kwa watoto kati ya mwaka moja hadi 12 ,vijana wenye umri kati ya 13- 19 ,wanawake walio kwenye umri wa kupata watoto na watu wanaoishi katika maeneo yenye minyoo. Hii ni njia mojawapo ya kupambana na utapiamlo, Anamia na matatizo yanayoletwa na minyoo.

  • Kufunga saum inafaidi afya yako vile vile nafsi yako ikiwa utafanya mara kwa mara

    26/01/2026 Duration: 10min

    Kuna ushahidi unaoonesha kwamba kufunga kunaweza kusaidia kurekebisha miili yetu ,wakati mwingine kuongeza maisha yetu, pia  njia bora ya kupunguza uzito,   Kitendo cha kukumbatia  Saum huchochea usafi wa moyo, nafsi na kusafisha mwili wako kwa kuondoa chakula ambacho mara nyingine hugeuka kuma sumu mwilini na chanzo cha magonjwa yasiyoambukiza.     Wataalam wa afya  pamoja na watetezi wa kufunga wanasema kuna uhusiano mkubwa kati ya afya ya kimwili na afya ya kiroho.   Kwenye makala hayo ya Siha Njema  tunakupa ufafanuzi huu tukisaidiwa na daktari  Julius Maleve na pia kiongozi wa kidini  Mtume Julius Suubi ,ambaye ameandika kitabu kuhusu faida za kufunga na ambaye amekuwa akifunga kwa kati ya siku 40 hadi 90 kila mwaka kwa zaidi ya mwaka 20 sasa.

  • Mpango wa kliniki tembezi unavyowafaidi wakaaji kaskazini mwa Kenya

    30/12/2025 Duration: 10min

    Mpango wa kliniki tembezi yaani mobile clinics  ni pale ambapo wahudumu wa afya wanatembea nyumba kwa nyumba na kuwatibu wenyeji kama vile wazee,akina mama na watoto.Maeneo ya kaskazini mwa Kenya ambapo hospitali  huwa mbali na vijiji ,ndiyo yanayolengwa kwenye mpango huo.

  • Juhudi za wazee kukomesha ukeketaji wa wasichana kaskazini mwa Kenya

    23/12/2025 Duration: 10min

    Ukeketaji wa wasichana bado ni changamoto kubwa katika baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa Kenya, licha ya marufuku ya kitaifa na juhudi za uhamasishaji zinazoendelea. Takwimu za Kitaifa KNBS na  zile Wizara ya Afya zinaonyesha kuwa asilimia 83 ya wanawake na wasichana wa Marsabit na 66 wa Isiolo tayari wamekeketwa—ikiziweka kaunti hizi miongoni mwa maeneo yenye viwango vya juu zaidi nchini.Sasa wazee maeneo hayo wameanza mchakato kukabiliana na ukeketaji huo

  • Je una uhakika wa usalama wa nyama unayoila kila mara nyumbani?

    17/12/2025 Duration: 10min

    Watalaam wa wanyama wanasisitiza wanyama wote wanaochinjwa ni sharti kutimiza viwango vya juu ikiwemo mwonekano ,afya  na usafi. Na kabla kuchinjwa wanyama hao kwa mfano ngombe ,hukaguliwa na kutengwa ili kubainisha nyama yao ni salama. Kwa mlaji unashauriwa kununua nyama iliyo na muhuri ambayo ni alama ya kuonesha nyama hiyo imekaguliwa na kuthibitishwa ni salama. Kwa wale wanaochinjia nyumbani bado unatakiwa kumpata mtalaam wa wanyama kumkagua mnyama wako na kutoa kibali cha kuchinjwa.

  • Mzigo wa usugu wa vimelea tishio kubwa kwa mifumo ya afya barani Afrika

    13/12/2025 Duration: 09min

    Matibabu mengi licha ya kupendekezwa au kuorodheshwa sahihi ,yanakabiliwa na usugu wa vimelea tatizo linalofanya dawa hizo kushindwa kutibu inavyotakikana Dawa za kutibu Malaria ,TB na Kipindu Pindu zimetajwa kuathirika sana ,haswa dawa aina ya antibiotics ambazo hutumika kuwa matibabu ya kwanza ya kuua vimelea.

  • Kwa nini ni muhimu kuwafikiria akina mama na watoto kwenye kampeni ya magonjwa yaliyosahaulika

    02/12/2025 Duration: 09min

    Ripoti nyingi huonesha kuwa idadi kubwa ya wagonjwa wanaougua magonjwa yaliyotengwa au kusahaulika ni akina mama au watoto  Hii ni kutokana na wao kutangamana moja kwa moja na mazingira ambayo huwa makazi ya vimelea vinavyosababisha magonjwa mbali mbali. Vimelea hao hukaa mchangani,kwenye maji au hupatikana kwenye kinyesi .

  • Mabadiliko ya tabia nchi yanayovyochochea magonjwa ya milipuko

    01/12/2025 Duration: 10min

    Tafiti zimeonesha kuwa magonjwa mengi ya milipuko haswa barani Afrika yanachochewa na mabadiliko ya tabia nchi Mafuriko ,ukame au kupanda joto yanaweza kusababisha kusambaa kwa haraka kwa vimelea vinavyosababisha magonjwa au kuzaana kwa haraka.

  • Mzigo wa ugonjwa wa Kisukari nchini Sudan Kusini unavyowawaliza wengi

    19/11/2025 Duration: 09min

    Sudan Kusini kando na kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa  wa Kisukari ,upatikanaji wa matibabu bado ni changamoto kubwa Watalaam nchini humo wanahoji mabadiliko ya mtindo wa maisha kama chanzo cha ongezeko la visa hivi.

  • Takwimu sahihi za mapema na maabara wezeshi kupambana na magonjwa ya milipuko

    12/11/2025 Duration: 09min

    WHO inashauri ukanda wa Afrika kuwekeza zaidi katika takwimu zilizo sahihi katika mikakati ya kupambana na magonjwa ya milipuko

  • Afueni kwa wanawake wanaokatwa matiti yao kutokana na saratani

    02/11/2025 Duration: 09min

    Kila mwezi wa Oktoba, ulimwengu huadhimisha Mwezi wa Uhamasishaji wa Saratani ya Matiti, lengo kuu likiwa kuhamasisha vipimo vya mapema ili kupunguza hatari ya ugonjwa huu na kutafuta msaada wa kifedha kwa ajili ya utafiti kuhusu saratani ya matiti. Inakadiriwa kuwa, wagonjwa wapya zaidi ya milioni 2.3 wa saratani ya matiti hugunduliwa kila mwaka, kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani. Wengi wa wanawake waliopatwa na saratani hii walilalzimika kukatawa titi moja au yote mawili ili kuokoa maisha yao,  na hivyo kupoteza kiungo muhimu cha mwili.

  • Kabla kuchagua,kununua mafuta ya kupikia ,zingatia mambo hayo

    30/10/2025 Duration: 10min

    Mafuta ya mzeituni, alizeti, mafuta ya nazi,mafuta ya mawese ni baadhi ya mafuta kula ambayo yanapendekezwa kutokana na namna yanavyotengenezwa. Mengi hutengenezwa  kwa kukamuliwa ,bila kuongezwa kemikali bila kutumia joto,hivyo ubora wake ni wa juu.   Mafuta haya hata hivyo ni ya bei juu sana na watalaam wanashauri badala ya kuchagua mafuta ambayo si mazuri na ambayo yanaweza kuongeza mafuta ya Cholesterol mwilini na kusababisha matatizo ya afya ,machaguo mbadala ni mafuta ya uto . Mafuta haya yanaweza kutokana na mimea au mbegu.   Mfano ni mafuta ya Parachichi,Karanga  na hata Canola. Aidha watalaam wanatoa tahadhari kuwa ukitumia mafuta yako kupika ,usipende kuyarudia au kutumia kwa zaidi ya mara moja  na usiyaweke mahali wazi maana yanayoweza kugeuka mabaya bila wewe kufahamu.

page 1 from 2