Habari Rfi-ki

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 3:59:34
  • More information

Informações:

Synopsis

Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.

Episodes

  • Mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Afrika kuzingatia usalama wa DRC

    13/02/2025 Duration: 10min

    Mkutano wa kila mwaka wa viongozi wa Afrika umeanza rasmi jijini Addis Ababa, #Ethiopia ambapo maswala muhimu ikiwemo usalama mashariki mwa #DRC, mapinduzi ya kijeshi na vita dhidi ya makundi ya kijihadi yakitarajiwa kugubika mkutano huu.Tulimuuliza mskilizaji natarajia nini kipya kutoka kwa viongozi wa AU? na iwapo anafikiri viongozi wameshindwa kumaliza changamoto za bara hili..

  • Kauli ya rais Donald Trump kuhamisha wapalestina yapingwa vikali

    12/02/2025 Duration: 10min

    Kwenye kipindi cha leo tunaangazia kauli  tata ya Rais Donald #trump, kuhusu mzozo wa #Gaza, safari hii akitishia kuvunjika kwa mkataba wa usitishaji mapigano, ikiwa Hamas haitawaachia mateka wote ifikapo Jumamosi ya wiki hii.Juma lililopita alidai kuwa nchi yake itachukua udhibiti wa Gaza na kuwahamisha Wapalestina.Tulimuuliza mskilizaji anazungumziaje kauli hiyo ya Trump and je huenda zikachochea mzozo zaidi kati ya #Israel na Hamas?

  • Hatua ya Kenya kuondoa mahojiano kwa waomba vitambulisho yaibua hisia mseto

    11/02/2025 Duration: 09min

    Makala haya yanaangazia hatua ya Serikali ya kenya  kusema  hakutakuwa na haja ya mahojiano kwa waomba vitambulisho toka katika maeneo ya mpakani, uamuzi ambao umeibua mjadala kuhusu masuala ya usalama.Tulimuuliza msikilizaji anazungumziaje hatua hiyo ya Kenya  vile vile nchini mwake hali ikoje

  • Kauli ya mkutano wa SADC na EAC kuhusu amani nchini DRC waibua maoni mseto

    10/02/2025 Duration: 09min

     kwenye makala ya leo tunaangazia  hatua ya  wakuu wa nchi za #SADC na EAC kutaka kusitishwa mapigano maramoja ,na kutaka  kuondoka kwa vikosi vya kigeni mashariki mwa #DRC, pamoja na Serikali ya Kinshasa kuzungumza moja kwa moja na waasi wa #M23 ambapo  wito huo  umepokelewa kwa hisia mseto na raia wa ukanda.

page 2 from 2