Synopsis
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.
Episodes
-
Umoja wa mataifa umesalia kimya ukiukaji wa haki ukiendelea
10/09/2025 Duration: 09minJe umoja wa mataifa umesalia kimya ukiukaji wa haki ukiendelea? Skiza makala haya kuskia hisia za waskilizaji wetu.
-
Raia wa nchi za Afrika wapendekeza watu wazima kupewa fursa ya kusoma na kuandika
10/09/2025 Duration: 09minKila mwaka tarehe 8 Septemba ulimwengu husherehekea maendeleo katika ujuzi wa kusoma na kuandika katika ngazi ya kimataifa, kikanda na kitaifa. Mwaka huu imekuwa ni fursa ya kutafakari kwa kina kuhusu maana ya kusoma na kuandika katika enzi hii ya kidijitali.
-
Kenya na Uganda zakubaliana rasmi kuondoa vizuizi vyote vya kibiashara
04/09/2025 Duration: 10minTunazungumzia hatua ya Kenya na Uganda kukubaliana rasmi kuondoa vizuizi vyote vya kibiashara, vikiwemo vizuizi vya ushuru na visivyo vya ushuru, ili kuwezesha mtiririko huru wa bidhaa, huduma, na watu kati ya mataifa hayo mawili
-
Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Tanzania zimeanza, wagombea wakinadi sera zao.
04/09/2025 Duration: 09minKampeni za uchaguzi mkuu wa Tanzania utakaofanyika tarehe 29 Oktoba zimeanza. Chama kikuu cha upinzani Chadema hakipo kwenye kampeni hizi, kufuatia msimamo wake wa kutaka mageuzi kwenye mfumo wa uchaguzi. Wasikilizaji wetu wanazungumzia aje kampeni hii na raia wa Tanzania wanatarajia sera gani kutoka kwa viongozi mbalimbali?
-
CHAN 2025: Nchi gani ilipendeza wasikilizaji wetu na maandalizi yalikuwa aje?
04/09/2025 Duration: 09minMichuano ya CHAN imemalizika rasmi mwishoni mwa juma, nchini Kenya, Morocco wakitawazwa mabingwa na Madagascar wakimaliza wa pili. Kuisha kwa michuano hii ni mwanzo wa maandalizi ya michuano ya AFCON itakayofanyika tena kwenye nchi za Kenya, Uganda na Tanzania mwaka 2027. Tumemuuliza msikilizaji wetu iwapo amefurahia michuano ya mwaka huu? Timu ipi ilikuwa bora kwake na kipi kifanyike kuelekea mashindano ya AFCON 2027.
-
-
-
Miaka kumi na mitano tangu Kenya kupata katiba mpya ambayo imetajwa endelevu
29/08/2025 Duration: 09min -
Mapigano kati ya FARDC na waasi wa M23 yanaendelea licha ya makubaliano ya amani
27/08/2025 Duration: 09min -
Je timu za nchi wenyeji wa CHAN zimefanyaje kwenye mchuoano wa CHAN 2024?
26/08/2025 Duration: 10minTimu za Kenya Uganda na Tanzania zimeaga mchuano katika hatua ya robo fainali
-
Michuano ya CHAN inaendelea je umeridhishwa kufikia sasa
23/08/2025 Duration: 10minMichuano ya CHAN inaendelea kuchezwa je umeridhishwa na michezo hiyo hadi kufikia sasa Skiza maoni ya mskilizaji.
-
Tanzania : Yabuni sheria kuwafungia nje wafanyakazi wageni
22/08/2025 Duration: 09minNchini Tanzania, nchi hiyo imebuni sheria kuwafungia nje wafanyakazi kutoka mataifa ya nje. Waskilizaji wetu walikuwa na haya ya kusema Skiza makala
-
Asasi za kiraia zamtaka rais William Ruto kuwataja hadharani wanaopokea rushwa
22/08/2025 Duration: 09minRais wa Kenya William Ruto, yupo kwenye shinikizo kubwa za kuwataja hadharani wabunge na Maseneta, aliodai wanapokea rushwa kutoka kwa Mawaziri na Magavana, asasi za kiraia zinasema hiyo ndio njia pekee ya kuwaaminisha wananchi kuwa, kiongozi huyo ana nia ya kupambana na ufisadi nchini humo.
-
Mzozo wa Ukraine: Rais Trump kujaribu kuwakutanisha rais Zelensky na rais Putin
22/08/2025 Duration: 09minBaada ya mkutano kati ya rais Donald Trump na rais Volodymyr zelensky na viongozi wa nchi za ulaya jijini Washington siku ya Jumatatu tarehe18 08 2025, Marekani sasa inajaribu kuwakutanisha rais Vladimir Putin na Zelensky ili kupata mwafaka wa mzozo wa Ukraine.
-
Rwanda: Wasichana kuanzia miaka 15 kupata huduma za uzazi wa mpango
20/08/2025 Duration: 09minMapema mwezi Agosti 2025 wabunge walipitisha sheria mpya itakayowaruhusu wasichana wa miaka 15 kupata huduma za uzazi wa mpango bila ruhusa ya wazazi, kwa lengo la kukabili mimba za utotoni. Awali sheria ya nchi hiyo ilikuwa inaruhusu wanawake wa miaka 18 pekee kupata huduma hizo.
-
Matarajio ya mkutano wa rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky jijini Washington DC nchini Marekani,
20/08/2025 Duration: 09minZelensky kuandamana na viongozi wa nchi za Ulaya kukutana na rais Donald Trump kujadili namna ya kumaliza uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
-
Nchini Kenya CAF yadhibiti idadi ya mashabiki viwanjani kwenye michezo ya chan
12/08/2025 Duration: 10minMada ya leo ni kuhuus michuano ya CHAN inapoendelea kushika kasi kwenye nchi za Kenya, Uganda na Tanzania, nchini Kenya baadhi ya mashabiki wamekuwa wakitumia nguvu kuingia uwanjani bila ya tiketi, hatua ambayo shirikisho la soka la Afrika CAF, limelazimika kupunguza idadi ya mashabiki kuingia uwanjani kwa sababu za kiusalama.,,tumemuuliza nini kifanyike kudhibiti usalama wa mashabiki na viwanja? na Kwenye nchi yako wakati wa mechi kubwa hali huwaje?
-
Leo ikiwa ni siku ya ijumaa tarehe 08 08 2025 huwa ni mada huru .
08/08/2025 Duration: 10minLeo ni siku ya mada huru. Tunampa nafasi mskilizaji kuchangia suala lolote ambalo limejiri nchini mwake wiki hii,na pia anaweza kuzungumzia kile ambacho amekisikia katika matangazo yetu ya juma hili.
-
Hatua ya wanasiasa kuhama hama vyama baada ya kukosa kufaulu kwenye uteuzi
07/08/2025 Duration: 10minmada ya leo ni kuhusu Nchini Tanzania ambapo baadhi ya wanasiasa wa CCM ambao hawakufaulu katika uteuzi wa chama, wameanza kuhamia vyama vingine ili kugombea viti mbalimbali kwenye uchaguzi wa oktoba mwaka huu.Hali hii imekuwa ikishuhudiwa pia katika mataifa mbalimbali barani Afrika. Tunamuuliza msikilizaji anaizungumziaje hatua hii ya hama hama kisiasa,na hali hii inashuhudiwa nchini mwake,,
-
Majadiliano ya Geneva kuhusu hatua za kukabiliana na matumizi ya plastiki
06/08/2025 Duration: 10minWawakilishi kutoka kote duniani wanakutana, wako Geneva, kujadili hatua za mwisho za kukabiliana na matumizi ya bidhaa za plastiki ambazo zimeendelea kuharibu mazingira.Tumemuuliza msikilizani ni njia zipi mbadala zitumike badala ya bidhaa za plastiki na anafikiri ni kwa nini nchi hazitaki kuachana na matumizi ya mifuko ya Plastiki.