Habari Za Un
Raia na hata wahudumu wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza wamekata tamaa
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:01:39
- More information
Informações:
Synopsis
Kadri siku zinavyozidi kusonga mbele, hali ya usalama na kibinadamu huko Ukanda wa Gaza inazidi kuzorota huku raia na hata wafanyakazi wa kutoa misaada wakisalia wamepigwa butwaa kwani mashambulizi kutoka Israeli yanaendelea kila uchao. Naanzia ndani ya hospitali ya Kamal Adwan kaskazini mwa Gaza, mtoto aliyejeruhiwa amebebwa akilia kwa uchungu. Kwingineko mgonjwa mwingine anatolewa kwenye gari la wagonjwa! Ni taswira iliyozoeleka sasa Gaza.Louise Wateridge ambaye ni Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Dharura katika shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa kutoka Gaza Kati amesema hali si hali.Anasema, “mambo kwa kweli yanazidi kuwa mabaya hapa. Kukata tamaa ni kila mahali. Namaanisha, watu unaozungumza nao, na wafanyakazi wenzangu niliozungumza nao hawajui sasa wafanye nini. Hawafahamu waende wapi. Unaweza kusikia nyuma yangu milio ya makombora ikiendelea.”Bi. Wateridge akaendelea kusema kuwa, “kutokuwa na matumaini ndio neno