Synopsis
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episodes
-
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "DAHARI"
22/05/2025 Duration: 36sKatika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "DAHARI."
-
22 MEI 2025
22/05/2025 Duration: 09minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini kumsikia mgeni wetu Prof. Wallah Bin Wallah, mwandishi mashuhuri wa vitabu vya Kiswahili kutoka Kenya ambaye anamulika umuhimu wa vitabu katika kukuza lugha ya Kiswahili. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno.Kwa mara ya kwanza tangu mwezi Februari, msaada wa kuokoa maisha umefika Gaza. Baada ya wiki 11 za kizuizi kutoka kwa mamlaka za Israeli, malori 198 yaliyobeba chakula, dawa na unga wa ngano yameingia leo kupitia mpaka wa Kerem Shalom kwa mujibu wa mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.Mratibu mkuu wa misaada wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, ameiitaja hatua hiyo kuwa ya muhimu sana, huku malori 90 yakipakuliwa usiku kwa ajili ya kusambazwa haraka.Mwaka 2024, vita havikuishia kwenye uwanja wa mapambano pekee vilivunja nyumba, masoko na shule. Kuanzia Gaza hadi Ukraine, Sudan hadi Myanmar na zaidi ya raia 36,000 walipoteza maisha yao katika mizozo 14 ya kivita kulimgana na ripoti ya Katibu Mk
-
Mapambano dhidi ya ndoa za kulazimishwa - Fatou Cissé
21/05/2025 Duration: 03minWakati ulimwengu ukiendelea kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia, tunaelekea nchini Mali, ambako Fatou Cissé, mkurugenzi wa filamu na mwanzilishi wa filamu iitwayo FURU, anatumia sanaa kuangazia suala zito la ndoa za kulazimishwa. Kupitia video maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa, tunapata simulizi hiyo inayohusu wasichana wawili waliokumbwa na changamoto hizi. Fatou anawapa wasichana wa Kiafrika sauti na jukwaa la kuzungumza hadharani kuhusu dhuluma wanazokumbana nazo. Sharon Jebichii anasimulia.
-
Mifuko iliyojazwa mchanga yafanikisha Barabara kupitika nchini Kenya
21/05/2025 Duration: 01minNchini Kenya, katika kaunti ya Meru hatua rahisi iliyochukuliwa inaleta mabadiliko makubwa na dhahiri kwani maeneo ambako awali barabara zilikuwa hazipitiki na hakuna mawasiliano, ubunifu wa kijapani umerejesha matumaini. Kulikoni? Assumpta Massoi anasimulia kupitia video ya Benki ya Dunia.
-
21 MEI 2025
21/05/2025 Duration: 09minHii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na mradi wa kutengeneza barabara katika kaunti ya Meru nchini Kenya. Makala tunaangazia simulizi ya mkurugenzi na mwanzilishi wa filamu iitwayo FURU, na mashinani tunakwenda Tanzania.Wafanyakazi wa misaada wa Umoja wa Mataifa leo wamesema kwamba bado wanangoja kibali kutoka kwa Israel ili kusambaza msaada wa kuokoa maisha ulioruhusiwa kuingia Gaza mwanzoni mwa wiki ambapo malori matano yalifanikiwa kuingia baada ya vikwazo kwa wiki 11.Nchini Kenya, katika kaunti ya Meru hatua rahisi iliyochukuliwa inaleta mabadiliko makubwa na dhahiri kwani maeneo ambako awali barabara zilikuwa hazipitiki na hakuna mawasiliano, ubunifu wa kijapani umerejesha matumaini.Katika makala wakati ulimwengu ukiendelea kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia, tunaelekea nchini Mali, ambako Fatou Cissé, mkurugenzi wa filamu na mwanzilishi wa filamu iitwayo FURU, anatumia sanaa kuangazia suala zito la ndoa za kulazimishwa.Na mashinani, fursa ni y
-
UN: Malori ya msaada Gaza bado yanasubiri ruhusa kusambaza chakula na dawa ndani ya eneo hilo
21/05/2025 Duration: 01minWafanyakazi wa misaada wa Umoja wa Mataifa leo wamesema kwamba bado wanangoja kibali kutoka kwa Israel ili kusambaza msaada wa kuokoa maisha ulioruhusiwa kuingia Gaza mwanzoni mwa wiki ambapo malori matano yalifanikiwa kuingia baada ya vikwazo kwa wiki 11. Flora Nducha na taarifa zaidi
-
20 MEI 2025
20/05/2025 Duration: 12minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika wafugaji wa nyuki nchini Tanzania leo ikiwa ni siku ya nyuki duniani iliyopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 20 Desemba mwaka 2017 kupitia azimio namba A/72/211.Baada ya miaka mitatu ya majadiliano, leo katika Mkutano wa Kimataifa wa Afya unaoendelea Geneva, Uswisi, nchi zimepitisha rasmi makubaliano ya kihistoria ya kuzuia, kujiandaa, na kukabiliana vyema na majanga ya magonjwa kwa siku zijazo. Taratibu zote zitakapopitishwa na angalau nchi 60, mkataba utaanza kutumika rasmi mwakani.Kutokana na mamlaka za Israeli kulegeza kwa muda mzingiro uliodumu kwa wiki 11, angalau sasa matumaini kidogo yamerejea Gaza, yameeleza leo mashirika ya Umoja wa Mataifa. Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya dharura, OCHA, Jens Laerke amesema tayari wamepata ruhusa ya kuyavusha malori matano yaliyokuwa yamezuiliwa jana.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP limetahadharisha leo kwamba bila ufadhili zaidi, huenda kati
-
Ufugaji nyuki katika Kaunti ya Kajiado umeleta manufaa kwa wenyeji - Bwana Mureithi
19/05/2025 Duration: 03minKesho ikiwa ni siku ya nyuki duniani ikimulika umuhimu wa nyuki tunakupeleka nchini Kenya, katika kijiji cha Embulmbul, ambapo mradi wa ufugaji nyuki uliofanikishwa na Shirika la Marekani la Misaada ya maendeleo, USAID, kwa kushirikiana na Idara ya Misitu ya Kenya, KFS na wadau wengine, umeleta tija kwa wenyeji. Mmoja wa wanufaika hao ni mwanamazingira Christopher Mureithi ambaye ni kiongozi wa kikundi cha kufuga nyuki katika msitu wa Ololua ambao wamefanikiwa sio tu kuboresha uzalishaji wa asali, bali pia kuchangia katika uhifadhi wa bioanuwai na misitu. Katika makala hii iliyoandaliwa na Sharon Jebichii Bwana Mureithi anaanza kwa kueleza mafanikio yao.
-
Simulizi ya Babu Jassim anayerejea nchini Syria kutoka Lebanon
19/05/2025 Duration: 02minTangu kuangushwa kwa utawala wa aliyekuwa Rais wa Syria Bashar al Assad aliyekuwa madarakani kwa zaidi ya muongo mmoja, wananchi wa Syria wamekuwa wakimiminika kurejea nchini mwao ambapo takwimu za sasa zinaonesha zaidi ya Wasyria 500,000 wamerejea kutoka nchi jirani. Mmoja wa waliorejea ni Babu Jassim na Leah Mushi anatuletea simulizi yake.
-
19 MEI 2025
19/05/2025 Duration: 11minHii leo jaridani tunaangazia masuala ya afya, na wakimbizi wa Syria wanaorejea nchini mwao. Makala tukwenda nchini Kenya kumulika ufukaji wa nyuki, na mashinani tunakuletea ujumbe wa Katibu Mkuu wa IMO kuhusu Siku ya Kimataifa ya wanawake mabaharia.Wajumbe kutoka kote duniani wamekusanyika mjini Geneva, Uswisi, kwa ajili ya Mkutano wa 78 wa Baraza la Afya Duniani (WHA78) unaofanyika kuanzia leo Mei 19 hadi 27 Mei mwaka huu.Tangu kuangushwa kwa utawala wa aliyekuwa Rais wa Syria Bashar al Assad aliyekuwa madarakani kwa zaidi ya muongo mmoja, wananchi wa Syria wamekuwa wakimiminika kurejea nchini mwao ambapo takwimu za sasa zinaonesha zaidi ya Wasyria 500,000 wamerejea kutoka nchi jirani. Mmoja wa waliorejea ni Babu Jassim na Leah Mushi anatuletea simulizi yake.Katika makala tunaelekea Kajiado nchini Kenya, ambako juhudi za utunzaji mazingira kupitia mradi wa ufugaji wa nyuki unaofadhiliwa na shirika la misaada la Marekani USAID kwa kushirikiana na idara ya misitu ya Kenya KFS hazichangii tu katika kukuza uchum
-
WHO: Mkutano wa 78 wa Baraza la Afaya Duniani umeng’oa nanga Geneva
19/05/2025 Duration: 02minWajumbe kutoka kote duniani wamekusanyika mjini Geneva, Uswisi, kwa ajili ya Mkutano wa 78 wa Baraza la Afya Duniani (WHA78) unaofanyika kuanzia leo Mei 19 hadi 27 Mei mwaka huu. Kaulimbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “Ulimwengu Mmoja kwa Afya” inaakisi dhamira ya pamoja ya kujenga mfumo wa afya wa kimataifa ulio imara, jumuishi na thabiti. Flora Nducha amefuatilia na hapa anatupasha zaidi
-
UN Women Tanzania yawawezesha wanawake wenye ulemavu kujiinua kiuchumi
16/05/2025 Duration: 05minShirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN WOMEN nchini Tanzania linaendesha mradi wa wanawake na uongozi chini ya ufadhili wa Finland mradi unaolenga kuwawezesha wanawake wenye ulemavu kujikwamua kiuchumi na pia kushiriki katika ngazi za uongozi katika maeneo yao.Kupitia makala hii Leah Mushi anatukutanisha na wanawake wawili walionufaika na mradi huo wa UN WOMEN na wanaeleza namna jamii zao zilivyokuwa kabla na baada ya kupatiwa elimu ya masuala mbalimbali yahusuyo watu wenye ulemavu.
-
FAO: Mikakati sahihi ya kilimo imeepusha mamilioni kutumbukia kwenye baa la njaa
16/05/2025 Duration: 02minUkosefu wa uhakika wa kupata chakula na utapiamlo kwa watoto uliongezeka kwa mwaka wa sita mfululizo mwaka 2024, na kuwatumbukiza mamilioni ya watu karibu na baa la njaa, huku wengine wakiepuka kutokana na misaada ya kimkakati. Imesema Ripoti ya Kimataifa kuhusu Janga la Chakula (GRFC) iliyotolewa leo huko Roma, Italia na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO. Flora Nducha anakutaarifu kwa muhtasari.
-
16 MEI 2025
16/05/2025 Duration: 12minHii leo jaridani tunaangazia uhakika wa chakula, na takwimu za afya za janga la COVID-19 kusababisha vifo, muda wa kuishi na hali ya afya na ustawi kwa ujumla. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani nchini DRC, kulikoni?Ukosefu wa uhakika wa kupata chakula na utapiamlo kwa watoto uliongezeka kwa mwaka wa sita mfululizo mwaka 2024, na kuwatumbukiza mamilioni ya watu karibu na baa la njaa, huku wengine wakiepuka kutokana na misaada ya kimkakati. Imesema Ripoti ya Kimataifa kuhusu Janga la Chakula (GRFC) iliyotolewa leo huko Roma, Italia na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO.Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) ya takwimu za afya duniani iliyochapishwa jana Mei 15 ikionesha athari kubwa zaidi za kiafya zilizosababishwa na janga la COVID-19 kuhusu vifo, muda wa kuishi na hali ya afya na ustawi kwa ujumla, imeweka wazi kuwa katika kipindi cha miaka miwili pekee, kati ya mwaka 2019 na 2021, matarajio ya kuishi yalipungua kwa mwaka mmoja na miezi nane ikiwa ni
-
WHO: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanachangia nusu ya vifo chini ya umri wa miaka 70
16/05/2025 Duration: 02minRipoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) ya takwimu za afya duniani iliyochapishwa jana Mei 15 ikionesha athari kubwa zaidi za kiafya zilizosababishwa na janga la COVID-19 kuhusu vifo, muda wa kuishi na hali ya afya na ustawi kwa ujumla, imeweka wazi kuwa katika kipindi cha miaka miwili pekee, kati ya mwaka 2019 na 2021, matarajio ya kuishi yalipungua kwa mwaka mmoja na miezi nane ikiwa ni maporomoko makubwa zaidi katika historia ya hivi karibuni hali iliyobatilisha mafanikio ya afya yaliyopatikana kwa muongo mmoja.
-
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "KIANGO."
15/05/2025 Duration: 52sKatika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno "KIANGO."
-
15 MEI 2025
15/05/2025 Duration: 09minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha katika mkutano wa CSW68 kumsikia Christina Kamili Ruhinda, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria nchini Tanzania, TANLAP. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno la wiki.Wakati dunia ikiadhimisha miaka 77 tangu Nakba ambapo zaidi ya wapalestina 700,000 walifurushwa kutoka vijiji na miji yao mwaka 1948, shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa Wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limetoa onyo kali kuhusu sura mpya ya mateso na ufurushwaji wa lazima uonaoendele Gaza.Akiwa na wasiwasi kutokana na ripoti za kuaminika kwamba wakimbizi wa Rohingya kutoka Myanmar walilazimishwa kushuka kutoka kwenye meli ya jeshi la wanamaji la India na kutoswa katika bahari ya Andaman wiki iliyopita, Mtaalamu wa UN wa Haki za Binadamu kuhusu wakimbizi wa Myanmar, ameanzisha uchunguzi kuhusu kitendo hicho alichoeleza kuwa ni cha kushangaza na kisichokubalika.Na baada ya muda mrefu kuonekana kama mchangiaji mkubwa wa uto
-
Wataalamu huru walaani mashambulizi ya kikatili dhidi ya wanawake na wasichana - Sudan
14/05/2025 Duration: 01minWataalamu huru wa haki za binadamu, leo Mei 14 wamekemea vikali ukiukwaji mkubwa na wa kimfumo dhidi ya wanawake na wasichana nchini Sudan ukiwemo ukatili wa kingono unaohusiana na vita, utekaji nyara, na mauaji, ambayo mengi yameripotiwa kufanywa na kundi la kijeshi la Rapid Support Forces (RSF). Anold Kayanda na taarifa zaidi.
-
Nyumba yetu ilivamiwa na tulilazimika kukimbia hadi hapa Burundi – Mkimbizi Charles
14/05/2025 Duration: 04minMapigano yanayoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, yamesababisha zaidi ya watu 70,000 kukimbia makazi yao na kuvuka mpaka kuingia nchi jirani ya Burundi wakitafuta usalama.
-
14 MEI 2025
14/05/2025 Duration: 10minHii leo jaridani tunaangazia haki za wanawake na wasichana nchini Sudan na hali ya kina mama na wanawake wajawazitio katika ukanda wa Gaza. Makala tukwenda nchini Burundi na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Wataalamu huru wa haki za binadamu, leo Mei 14 wamekemea vikali ukiukwaji mkubwa na wa kimfumo dhidi ya wanawake na wasichana nchini Sudan ukiwemo ukatili wa kingono unaohusiana na vita, utekaji nyara, na mauaji, ambayo mengi yameripotiwa kufanywa na kundi la kijeshi la Rapid Support Forces (RSF).Huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli, wanawake na wasichana wakiwemo wanawake wajawazito na wale waliojifungua, wamelazimika kukimbia makazi yao na wanaishi katika mazingira hatarishi bila huduma za msingi za kiafya. Sharon Jebichii anaangazia simulizi ya mama mmoja, mkazi wa kambi ya wakimbizi ya Jabalia, Kaskazini mwa Gaza, ambaye alijifungua akiwa amekimbia vita,na sasa anahangaika kumtunza binti yake mchanga.Katika makala Assumpta Massoi kwa makala hiyo na zaidi ya yote shirika la Umoja wa M