Synopsis
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episodes
-
Jifunze Kiswahili: Maana za neno "FIFILIZA"
10/04/2025 Duration: 51sKatika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana za neno "FIFILIZA"
-
10 APRILI 2025
10/04/2025 Duration: 09minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo Idhaa hii inazungumza na Mwenyekiti wa Tanzania Women Ecocomic Empowerment Network (TAWEN), ambaye pia ni mchumi mbobezi Bi. Janet Zebedayo Mbene. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na neno la wiki.Shukran Anold na leo tunaanzia huko Geneva Uswisi ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limetoa muongozo wake wa kwanza duniani wa kutambua, kutoa matibabu kwa haraka na matibabu ya muda mrefu kwa ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo.Nchini Chad katika mpaka wake na Sudan ambako Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi ametembelea na kuzungumza na wakimbizi wa Sudan pamoja na kujionea hali zao wakati huu ambapo wamepunguza kutoa chakula, malazi , maji na dawa na kauli yake ikawa moja tu, “Ninatoa wito kwa wafadhili, tafadhali msipunguze msaada kwa wathirika wa vita vya Sudan.”.Taarifa ya pamoja ya mashirika ya kibinadamu inayotolewa kila baada ya wiki mbili imeeleza kuhusu hali katika Ukanda wa Gaza
-
UNICEF na wadau Kenya waelekea kufanikisha ndoto ya Sharlyne kuwa mwandishi wa habari
09/04/2025 Duration: 04minKutana na Shalyne Kaputa, mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 16 kutoka kaunti ya Turkana, Kaskazini-Magharibi mwa Kenya. Tofauti na shangazi yake, ambaye hakuweza kuendelea na elimu yake kutokana na kukosa karo, yeye anasoma elimu ya sekondari sasa ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa mwandishi wa habari. Yote yanawezekana kutokana na mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa msaada wa shirika la Norway la Maendeleo NORAD na wadau wengine. Je ni usaidizi gani wanapatiwa? Ungana na Assumpta Massoi.
-
Lazima hatua madhubuti zichukuliwe kukomesha mzunguko wa watu kutoweka nchini Sudan - Radhouane Nouicer
09/04/2025 Duration: 03minWakati hofu ikiendelea kuhusu watu kutoweka kwa wingi nchini Sudan, Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa aliyeteuliwa na Ofisi ya Haki za Binadamu OHCHR anayehusika na haki za binadamu nchini humo Radhouane Nouicer ametoa wito wa dharura kuhusu hali ya raia waliokwama katika vita kubwa nchini humo. Flora Nducha na taarifa zaidi.
-
09 APRILI 2025
09/04/2025 Duration: 12minHii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika katika jimbo la Upper Nile nchini Sudan, na haki za binadamu na watu kutoweka kwa wingi nchini Sudan. Makala inatupeleka nchini Kenya na Mashinani tunakwenda Gaza, kulikoni?Nchini Sudan Kusini, familia zilizo kwenye hali duni katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ziko katika hali tete sana huku mapigano yakizidi kuongezeka na njaa ikikaribia kufikia viwango vya juu kabisa, limeonya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP).Wakati hofu ikiendelea kuhusu watu kutoweka kwa wingi nchini Sudan, Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa aliyeteuliwa na Ofisi ya Haki za Binadamu OHCHR anayehusika na haki za binadamu nchini humo Radhouane Nouicer ametoa wito wa dharura kuhusu hali ya raia waliokwama katika vita kubwa nchini humo.Katika inatupeleka nchini Kenya kufuatilia simulizi ya Shalyne Kaputa, mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 16 kutoka kaunti ya Turkana ambaye tofauti na shangazi yake ambaye hakuweza kuendelea na elimu ya
-
Ukosefu wa usalama wanyima chakula wahitaji Upper Nile nchini Sudan Kusini
09/04/2025 Duration: 01minNchini Sudan Kusini, familia zilizo kwenye hali duni katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ziko katika hali tete sana huku mapigano yakizidi kuongezeka na njaa ikikaribia kufikia viwango vya juu kabisa, limeonya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP). Anold Kayanda na maelezo zaidi.
-
08 APRILI 2025
08/04/2025 Duration: 11minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika shughuli za shirika lisilo la kiserikali la KINNAPA Development Programme la huko nchini Tanzania katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu likijikita zaidi katika usawa wa kijinsia. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani:Uganda, ambayo tayari ni mwenyeji wa wakimbizi wengi zaidi barani Afrika, inakabiliwa na shinikizo kubwa baada ya wakimbizi zaidi ya 41,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kuingia nchini humo tangu Januari mwaka huu, wakikimbia machafuko mapya mashariki mwa nchi yao limesema leo Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. UNHCR imesema watu walioko katika mazingira hatarishi wanatambuliwa kwa msaada maalum, huku familia zilizotengana zikisaidiwa kuunganishwa tena.Siku kumi baada ya matetemeko ya ardhi ya kutisha yaliyoitikisa Myanmar tarehe 28 Machi, idadi ya vifo inaendelea kuongezeka. Titon Mitra, Mwakilishi wa Kikanda wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP nchini humo, akir
-
Dayspring Foundation nchini Tanzania yatekeleza kivitendo dhana ya UN ya michezo kwa maendeleo
07/04/2025 Duration: 04minSiku ya kimataifa ya Michezo kwa ajili ya Maendeleo na Amani imeadhimishwa tarehe 6 mwezi huu wa Aprili maudhui yakiwa Ujumuishaji wa kijamii, hususan makundi ya pembezoni. Umoja wa Mataifa kupitia wavuti wake unasema kuwa siku hii inatambuliwa kutokana na nafasi ya michezo katika kuleta mabadiliko chanya, kuondoa vikwazo na kuvuka mipaka. Na usuli wa maudhui ya mwaka huu ni kwamba fikra potofu kwenye jamii zimesababisha baadhi ya watu kutokana na jinsia yao, umri, au rangi wanashindwa kushiriki kwenye michezo ambayo kwa njia moja au nyingine hutokomeza umaskini kwa kuwezesha washiriki kujipatia kipato. Nchini Tanzania shirika la kiraia la Dayspring Foundation limetambua nafasi ya michezo na limeanza kuchukua hatua. Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Rosemary Mwaipopo ambaye anaanza kwa kuelezea ni kwa nini waliamua kujikita katika kusaka vipaji.
-
Kwibuka2025: Katibu Mkuu UN ahimiza mshikamano wa kimataifa dhidi ya chuki
07/04/2025 Duration: 02minDunia inapokumbuka miaka 31 tangu mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma ujumbe mzito wa maombolezo na onyo, akitaka mshikamano wa kimataifa kupambana na ongezeko la chuki, mgawanyiko, na misimamo mikali kupitia mifumo ya kidijitali. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
-
07 APRILI 2025
07/04/2025 Duration: 11minHii leo jaridani tunaangazia makumbusho ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, na Siku ya Afya Duniani. Makala inamulika nafasi ya michezo katika kusongesha amani na maendeleo, na mashinani tunakwenda nchini Kenya, kulikoni?Dunia inapokumbuka miaka 31 tangu mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma ujumbe mzito wa maombolezo na onyo, akitaka mshikamano wa kimataifa kupambana na ongezeko la chuki, mgawanyiko, na misimamo mikali kupitia mifumo ya kidijitali.Leo ni Siku ya Afya Duniani ambayo mwaka huu inangazia suala muhimu kwa afya ya dunia, changamoto maalum wanazokumbana nazo wanawake na wasichana lakini pia vifo vya watoto wachanga, na ili kuhakikisha changamoto hizo zinashughulikiwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO limezindua kampeni ya mwaka mzima ya “Mwanzo wenye afya ni mustakbali wenye matumaini”..Makala inamulika nafasi ya michezo katika kusongesha amani na maendeleo, ambapo Assump
-
Hatua za haraka zinahitajika sasa kuzuia vifo na kulinda afya ya wanawake na wasichana: UN
07/04/2025 Duration: 02minLeo ni Siku ya Afya Duniani ambayo mwaka huu inangazia suala muhimu kwa afya ya dunia, changamoto maalum wanazokumbana nazo wanawake na wasichana lakini pia vifo vya watoto wachanga, na ili kuhakikisha changamoto hizo zinashughulikiwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO limezindua kampeni ya mwaka mzima ya “Mwanzo wenye afya ni mustakbali wenye matumaini”. Flora Nducha anafafanua zaidi.
-
Uongozi bora na matumizi bora ya rasilimali vitaikomboa Afrika kimaendeleo: Vijana Kenya
04/04/2025 Duration: 03minMajadiliano ya siku mbili yanayofanyika kila mwaka ya será kuhusu maendeleo endelevu. Majadiliano hayo yanayokunja jamvi leo jijini Nairobi Kenya yameandaliwa na Club De Madrid na mwaka huu yakijikita na ufadhili wa maendeleo na kuwaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wastaafu w anchi na serikali, wadau wa maendeleo na vijana. Stella Vuzo kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi amepata fursa ya kuzungumza na baadhi ya vijana wanaoshiriki mkutano huo wa club de Madrid je wanasemaje? Ungana nao katika makala hii
-
Umoja wa Mataifa kuendelea kuisaidia Somalia kuonda mabomu ya kutegwa ardhini
04/04/2025 Duration: 01minIkiwa leo ni Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini na Msaada wa Hatua Dhidi ya Mabomu hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akisisitiza mataifa duniani kote kuheshimu mikataba ya kimataifa dhidi ya vilipuzi na silaha nyingine, Umoja wa Mataifa leo umethibitisha tena dhamira yake ya kusaidia Somalia katika mapambano dhidi ya hatari za vilipuzi kwa ajili ya mustakabali salama kwa Wasomali wote. Anold Kayanda na taarifa zaidi.
-
04 APRILI 2025
04/04/2025 Duration: 09minHii leo jaridani tunaangazia Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini. Makala inamulika harakati za kusongesha malengo ya maendeleo endelevu ikitupeleka nchini Kenya na mashinani tunasalia huko huko nchini Kenya, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini na Msaada wa Hatua Dhidi ya Mabomu hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akisisitiza nchi kuheshimu mikataba ya kimataifa dhidi ya vilipuzi na silaha nyingine, Umoja wa Mataifa leo umethibitisha tena dhamira yake ya kusaidia Somalia katika mapambano dhidi ya hatari za vilipuzi kwa ajili ya mustakabali salama kwa Wasomali wote.Mwaka huu wa 2025, Siku ya Kimataifa ya Uhamasishaji Kuhusu Mabomu ya Ardhi na Usaidizi kwa Hatua Dhidi ya Mabomu inaadhimishwa chini ya kaulimbiu “Mustakabali Salama Unaanzia Hapa.” Umoja wa Mataifa inasisitiza umuhimu wa kufadhili miradi midogo yenye athari za haraka kusaidia watu wenye ulemavu wa viungo waliathirika katika mizozo. Juhudi hizi zinaimarisha u
-
Uteguaji mabomu ya ardhini ni suala la amani na kiutu - UNMAS
04/04/2025 Duration: 02minIkiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini, kauli mbiu ikiwa Mustakabali salama unaanzia hapa, Umoja wa Mataifa unasisitiza umuhimu wa kufadhili miradi midogo yenye matokeo chanya na ya haraka ili kusaidia sio tu watu wanaopata ulemavu wa viungo kutokana na madhara ya mabomu hayo bali pia kuwezesha watu kurejea kwenye maisha yao ya kawaida Sharon Jebichii anamulika Lebanon na Libya.
-
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "MHARUMA.”
03/04/2025 Duration: 31sKatika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MHARUMA.”
-
03 APRILI 2025
03/04/2025 Duration: 11minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha kwenye mkutano wa hivi majuzi wa CSW69 kufuatilia harakati za Mfuko wa CRDB za kujengea uwezo na kuinua wanawake nchini Tanzania. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno “MHARUMA.”Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wa misaada ya kibinadamu leo wamesema wanaendelea kuwasaidia watu wa Muyanmar na mahitaji ya msingi baada ya tetemeko kubwa la ardhi la Ijuma iliyopita ambapo idadi ya waliopoteza maisha sasa ni zaidi ya 2,800, maelfu wamejerihiwa na mamia bado hawajulikani wako.Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk, amesema leo kwamba ameshtushwa na ripoti za mauaji ya raia bila kufuata utaratibu wa kisheria yaliyoenea mjini Khartoum baada ya kurejeshwa kwa mji huo chini ya udhibiti wa Jeshi la Sudan (SAF) tarehe 26 Machi.Na majadiliano ya siku mbili ya kila mwaka ya será kuhusu maendeleo endelevu yaliyoandaliwa na Club De Madrid yameanza leo Nairobi Kenya mwaka huu yakijikita na ufadhili wa maendeleo. shudu
-
UN na wadau wasadie chanzo cha usonji kifahamike - Lukiza Foundation
02/04/2025 Duration: 04minHii leo dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu usonji, Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imezungumza na Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lukiza Foundation nchini Tanzania inayoelimisha umma kuhusu usonji. Usonji ni hali inayompata mtoto au utofauti au changamoto katika mfumo wake wa ufahamu na ubongo na kusababisha changamoto za kimawasiliano, tabia na kudhibiti hisia mwili. Hoja kubwa ni kwamba hadi sasa sababu ya hali hiyo kumpata mtoto haijajulikana na ndipo taasisi hiyo inachagiza Umoja wa Mataifa na wadau washikamane katika tafiti kujua chanjo kama njia mojawapo ya kudhibiti au kutibu ugonjwa huo. Basi kwa kina kufahamu harakati za taasisi hiyo nchini Tanzania, nampisha Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.
-
Ujumbe wa Katibu Mkuu UN Siku ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma Kuhusu Usonji
02/04/2025 Duration: 01minKatika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma kuhusu Usonji (Autism) mwaka huu wa 2025, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesisitiza umuhimu wa ujumuishaji na usawa kwa watu wenye changamoto hiyo akitambua mafanikio yao pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo duniani kote. Anold Kayanda anaeleza zaidi.
-
02 APRILI 2025
02/04/2025 Duration: 09minHii leo jaridani tunaangazia Siku ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma kuhusu Usonji, na wakimbizi wa ndani nchini DRC. Makala inatupeleka nchini Tanzania kwa mada hiyo hiyo ya elimu kuhusu usonji, na mashinani tunakwenda Gaza.Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma kuhusu Usonji (Autism) mwaka huu wa 2025, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesisitiza umuhimu wa ujumuishaji na usawa kwa watu wenye changamoto hiyo akitambua mafanikio yao pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo duniani kote.Jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Thérèse Kavira, mwanamke shupavu aliyelazimika kukimbilia mji wa Beni baada ya waasi kuvamia kijiji chake sasa ameona nusu kwenye maisha yake kufuatia mafunzo ya kuoka mikate yaliyotolewa na ofisi ya Utafiti na Usaidizi kwa Mahusiano ya Kimataifa nchini humo pamoja na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani DRC, MONUSCO na sasa anajikimu kimaisha.Makala leo kama tulivyokujulisha ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umm