Habari Za Un

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 8:57:07
  • More information

Informações:

Synopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodes

  • Kutana na Celestin Mbaruku mkimbizi mnufaika wa Mpango wa Utambuzi wa Ujuzi wa Awali nchini Kenya

    28/02/2025 Duration: 03min

    Kama mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Celestin Mbaruku hakuwa na fursa ya ajira rasmi hadi alipothibitishwa ujuzi wake kupitia mpango wa Serikali ya Kenya wa Utambuzi wa Ujuzi wa Awali, uliotengenezwa kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO.Kupitia ILO Celestin Mbaruku ni mnufaika wa ufadhili wa PROSPECTS, ushirikiano wa kimataifa unaojumuisha mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa ukilenga kuboresha upatikanaji wa elimu, ulinzi wa jamii, na ajira yenye hadhi kwa jamii zinazowakaribisha wakimbizi na watu waliolazimika kuhama makazi yao.Kimakosa, Celestin Mbaruku akiwa nchini mwake DRC alidhaniwa kuwa muasi, akafungwa lakini akamudu kutoroka hadi Kenya.Kabla ya masaibu haya, huko DRC alikuwa Mwalimu anayesimamia nidhamu katika shule alikokuwa anafanya kazi ya lakini kwa kuwa vyeti vyake vilipotea, hata alipovuka kuingia Kenya, hakuwa na uthibitisho wa kiwango cha elimu yake licha ya kuwa ana diploma ya mbinu za ufundishaji.Na hapo ndipo ikabidi achomoe kibin

  • Guterres: Mwezi Mtukufu wa Ramadhani utumike kuleta amani

    28/02/2025 Duration: 02min

    Kuelekea kuanza kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwishoni mwa wiki hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma ujumbe wake wa kutaka kipindi hicho cha takribani siku 30 kitumike kuleta amani na kuongoza kuelekea dunia yenye yenye haki na huruma zaidi. Selina Jerobon na taarifa zaidi.

  • 28 FEBRUARI 2025

    28/02/2025 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia migogoro ambayo yameendelee kwa muda mrefu Sudan Kusini, na ujumbe wa Katibu Mkuu ikielekea kuanza kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Makala inatupeleka nchini Kenya, na mashinani nchini Tanzania.Viongozi wa kisiasa wa Sudan Kusini lazima wakabiliane na ukwepaji wa sheria na ufisadi unaochochea ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, la sivyo watahatarisha mpito wa kisiasa wa nchi hiyo, imesema Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Sudan Kusini katika ripoti yake iliyotolewa leo.Kuelekea kuanza kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwishoni mwa wiki hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma ujumbe wake wa kutaka kipindi hicho cha takribani siku 30 kitumike kuleta amani na kuongoza kuelekea dunia yenye yenye haki na huruma zaidi..Katika makala Anold Kayanda wa Idhaa hii kutokana na video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, anakupeleka nchini Kenya kukutanisha na mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC am

  • Viongozi wabainika kuwa chanzo cha kutomalizika kwa mzozo nchini Sudan Kusini

    28/02/2025 Duration: 02min

    Viongozi wa kisiasa wa Sudan Kusini lazima wakabiliane na ukwepaji wa sheria na ufisadi unaochochea ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, la sivyo watahatarisha mpito wa kisiasa wa nchi hiyo, imesema Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Sudan Kusini katika ripoti yake iliyotolewa leo kama anavyoripoti Flora Nducha.

  • Jifunze Kiswahili: Maana ya methali “Fahari isiyo pari haina heri"

    27/02/2025 Duration: 01min

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “FAHARI ISIYO PARI HAINA HERI.”.

  • 27 FEBRUARI 2025

    27/02/2025 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayokupeleka nchini DRC ambako leo tunamulika mmoja wa raia aliyerejea makazi yake huko Sake, nje kidogo ya mji wa Goma, jimboni Kivu Kaskazini baada ya waasi wa M23 kutangaza kuwa wakimbizi wote wa ndani lazima warejee vijijini kwao. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa methali.Ikiwa ni mwezi mmoja sasa tangu waasi wa M23 watwae mji wa Goma jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na kuendelea kutwaa miji mingine huku mamia ya maelfu ya watu wakifurushwa makwao, hii leo mashirika ya Kibinadamu nchini humo yametoa ombi la dola bilioni 2.54 ili kusaidia watu milioni 11 walioathiriwa vibaya na mzozo unaoendelea.Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO Dkt. Tedros Ghebreysus ametangaza kuwa ugonjwa wa mpox bado ni tishio la afya ya umma duniani na hivyo nchi lazima ziendelee kuwa makini katika ufuatiliaji, uchunguzi, kinga na matibabu.Na kuelekea Mkutano wa viongozi kuhusu Mifumo ya uzalishaji

  • Hatari ya watu milioni 4.4 nchini Somalia kukumbwa na njaa mwezi Aprili mwaka huu

    26/02/2025 Duration: 02min

    Watu milioni 4.4 nchini Somalia wako hatarini kukumbwa na njaa ifikapo mwezi Aprili mwaka huu wa 2025, kutokana na ukame mkali, mizozo na ongezeko kubwa la bei za vyakula. Selina Jerobon na taarifa zaidi..

  • 26 FEBRUARI 2025

    26/02/2025 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu nchini Somalia na huduma zaa faya kwa wakimbizi wajawazito nchini Chad. Makala inatupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Uganda, kulikoni?Watu milioni 4.4 nchini Somalia wako hatarini kukumbwa na njaa ifikapo mwezi Aprili mwaka huu wa 2025, kutokana na ukame mkali, mizozo na ongezeko kubwa la bei za vyakula.Nchini Chad, taifa lililoko kaskazini-kati mwa Afrika mkunga mmoja amehamia kwa muda katika kambi ya wakimbizi ili kuhakikisha wajawazito wanapata huduma bora kabla na baada ya kujifungua kama njia mojawapo ya kuepusha vifo vya wajawazito na watoto wachanga.Makala inatupeleka nchini Kenya kumulika mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, wa kulinda lishe ya wasiojiweza unavyoleta mabadiliko katika  jamii kuanzia kaunti ya Turkana hadi kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma.Katika mashinani fursa ni yake Dkt Annett Alenyo Ngabirano kutoka Uganda akisema juhudi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO na Wizara ya Afya ya Ug

  • Mradi wa FAO wa kulinda lishe ya wasiojiweza umekuwa mkombozi Turkana nchini Kenya

    26/02/2025 Duration: 04min

    Mradi unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, wa kulinda lishe ya wasiojiweza wakiwemo wajasiriamali wa bishara ndogodogo na za kati, wakulima wadogo wa matunda na mbogamboga, wafugaji  na wachuuzi wa samaki kama sehemu ya jitihada za kujikwamua baada ya janga la COVID-19 umeleta nuru kwa jamii mbalimbali ikiwemo katika kaunti ya Turkana Kaskazini Magharibi mwa Kenya na katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma. Je unawanufaisha vipi wakulima na kwa nini ni muhimu? Ungana na Flora Nducha katika makala hii kwa undani zaidi

  • Mkunga apiga kambi kwa wakimbizi ili kuepusha vifo vya wajawazito - Chad

    26/02/2025 Duration: 01min

    Nchini Chad, taifa lililoko kaskazini-kati mwa Afrika mkunga mmoja amehamia kwa muda katika kambi ya wakimbizi ili kuhakikisha wajawazito wanapata huduma bora kabla na baada ya kujifungua kama njia mojawapo ya kuepusha vifo vya wajawazito na watoto wachanga. Taarifa ya Evarist Mapesa inafafanua zaidi.

  • 25 FEBRUARI 2025

    25/02/2025 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DRC ambako ghasia za hivi karibuni huko Goma zimeongeza mahitaji ya huduma za afya, WHO imechangia vifaa muhimu vya matibabu ili kukabialiana na hali hiyo. Pata pia muhtasari wa habari na mashinani.Kufuatia ripoti za kuweko kwa ugonjwa usiojulikana huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambao tayari umeambukiza mamia ya watu na kusababisha makumi ya vifo, shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, limesema bado linaendelea na uchunguzi wa ugonjwa huo uliotangazwa kwa chapisho la kikanda la WHO.Kampeni ya chanjo ya polio inayoendelea ukanda wa Gaza kwa lengo la kudhibiti kusambaa kwa virusi vya polio na kuzuia tishio la ugonjwa huo kusambaa maeneo mengine na nchi jirani, imekuwa na mafanikio makubwa kwani hata eneo la Gaza Kaskazini, mwitikio ulikuwa mkubwa licha ya mvua na baridi kali.Na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP hii leo limetangaza kuwa sitisho la mapigano Gaza limewezesha kufikisha eneo hilo kwa wa

  • Gaza: Awamu ya tatu ya chanjo dhidi ya polio inaendelea

    24/02/2025 Duration: 03min

    Katika makala hii Anold Kayanda wa Idhaa hii anaangazia chanjo inayoendelea katika Ukanda wa Gaza dhidi ya polio chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya ya Palestina kwa kusaidiwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa. Uchanjaji huu wa sasa kwa njia ya matone dhidi ya polio ni wa dharura kutokana na kugunduliwa kwa virusi vya polio katika sampuli za maji taka huko Gaza hivi karibuni, ikionesha kuwa virusi hivyo vinaendelea kuzunguka katika mazingira na hivyo kuwaweka watoto katika hatari. 

  • UNICEF na WFP wawezesha watoto nchini Sudan Kusini kwenda shule ili watimize ndoto zao

    24/02/2025 Duration: 02min

    Mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la Kuhudumia Watoto, UNICEF na la Mpango wa Chakula duniani, WFP kwa kushirikiana na mradi wa pamoja wa kimataifa wa mnepo ,au Joint Resilience Project (JRP) nchini Sudan Kusini ,wanatekeleza msaada wa chakula bora na salama bila malipo kwa watoto shuleni ,kwa zaidi ya wanufaika laki tano alfu Hamsini 550,000 ili kuhakikisha ndoto za watoto hao zinatimia. Ni sauti ya watoto wakitembea kuelekea shuleni huku wakiwa wamevibeba vitabu vyao mikononi.Kupitia video iliyoandaliwa na UNICEF, Tieng Maleng, mnufaika wa mradi wa JRP kutoka kijiji cha Pangapdit anaonekana akiwapa watoto wake kiamsha kinywa huku wakiwa wamekaa nje ya boma lao wakiwa wamevalia sare zao tayari kwenda shule. Kwa furaha anaeleza jinsi mradi huu umekuwa wa manufaa kwa familia yake.“Baada ya kupokea msaada wa kifedha, nilitumia fedha kidogo kulipa ada ya shule ya watoto wangu. Nikachukua sehemu kidogo ya fedha hizo kununua viatu vyao, na dawa. Pia nilitumia sehemu nyingine ya msaada huo katika kilimo

  • 24 FEBRUARI 2025

    24/02/2025 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia miaka mitatu ya vita nchini Ukraine, machafuko nchini DRC na elimu Sudan Kusini. Makala inatupeleka katika ukanda wa Gaza kumulika harakati za chanjo ya polio, na mashinani nchini Kenya kusikia ujumbe kuhusu umuhimu wa lugha mama.Mkutano wa 58 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu umeanza leo jijini Geneva, Uswisi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezungumzia kiza kilichotanda duniani hivi sasa kutokana na mapigano  yanayoendelea sehemu mbalimbali kuanzia Ukraine, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC  hadi Ukanda wa Gaza, yakiambatana na ukiukwaji mkubwa wa haki, akitaka kila juhudi zichukuliwe kusaka amani ya kudumu.Huko Gaza Kaskazini, kwenye eneo la wapalestina linalokaliwa na Israeli, wanafamilia zilizofurushwa makwao kutokana na vita kati ya Israeli na wanamgambo wa Hamas wanavumilia msimu wa baridi kali katika makazi ya muda ya mahema yanayopigwa na upepo na mvua usiku na mchana, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia

  • Ukraine: Miaka 3 ya kumbukumbu mbaya, juhudi zifanyike mzozo uishe - Guterres

    24/02/2025 Duration: 02min

    Mkutano wa 58 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu umeanza leo jijini Geneva, Uswisi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezungumzia kiza kilichotanda duniani hivi sasa kutokana na mapigano  yanayoendelea sehemu mbalimbali kuanzia Ukraine, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC  hadi Ukanda wa Gaza, yakiambatana na ukiukwaji mkubwa wa haki, akitaka kila juhudi zichukuliwe kusaka amani ya kudumu. Selina Jerobon na taarifa kamili..

  • Hofu ya raia zaidi kukimbia DRC kuelekea Burundi, UNHCR yasaka dola milioni 40.4 za kuwasaidia

    21/02/2025 Duration: 02min

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR limetoa ombi la dola milioni 40.4 ili kujiandaa na kutoa huduma za kuokoa maisha na usaidizi kwa wakimbizi wa ndani na waliokimbilia nchi jirani baada ya wakati huu ambapo mashambulizi ya waasi wa M23 yanazidi kufurusha raia kutoka Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokraia ya Congo, DRC. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

  • Maelfu wavuka mto Rusizi kwa mtumbwi kutoka DRC na kuingia Burundi ili kuokoa maisha yao

    21/02/2025 Duration: 05min

    Maelfu ya watu wanawasili nchini Burundi, wakikimbia mapigano yanayozidi kushamiri huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hususan katika majimbo ya Kivu Kusini na Kivu Kaskazini. Waasi wa M23 wanaendelea kupanua wigo wa maeneo wanayomiliki, hali inayotumbukiza raia kwenye changamoto za usalama, na kulazimu wale wanaoweza kukimbia. Wengine wameuawa, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, na majeruhi wako hospitalini ambako huduma nazo zimedorora kwani M23 wamefunga barabara katika maeneo yote wanayodhibiti. Lakini wale wanaokimbilia Burundi hali yao iko vipi? Evarist Mapesa anakusimulia zaidi kupitia video iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.

  • 21 FEBRUARI 2025

    21/02/2025 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia mahitaji ya wakimbizi wanaokimbia machafuko DRC wakielekea nchini Burundi, na hali ya wakimbizi wa ndani Gaza wakati huu wa msimu wa baridi. Makala tunakurejesha nchini DRC na mashinani tunakwenda nchini Tanzania.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR limetoa ombi la dola milioni 40.4 ili kujiandaa na kutoa huduma za kuokoa maisha na usaidizi kwa wakimbizi wa ndani na waliokimbilia nchi jirani baada ya wakati huu ambapo mashambulizi ya waasi wa M23 yanazidi kufurusha raia kutoka Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokraia ya Congo, DRC.Huko Gaza Kaskazini, kwenye eneo la wapalestina linalokaliwa na Israeli, wanafamilia zilizofurushwa makwao kutokana na vita kati ya Israeli na wanamgambo wa Hamas wanavumilia msimu wa baridi kali katika makazi ya muda ya mahema yanayopigwa na upepo na mvua usiku na mchana, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF. Nyumba zao zimeharibika na kuacha watoto kuishi katika mazingira mabaya.Katika makala Evarist Map

  • Watoto watota kwa mvua katika ukanda Gaza, huku baridi kali ikitishia afya zao

    21/02/2025 Duration: 02min

    Huko Gaza Kaskazini, kwenye eneo la wapalestina linalokaliwa na Israeli, wanafamilia zilizofurushwa makwao kutokana na vita kati ya Israeli na wanamgambo wa Hamas wanavumilia msimu wa baridi kali katika makazi ya muda ya mahema yanayopigwa na upepo na mvua usiku na mchana, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF. Nyumba zao zimeharibika na kuacha watoto kuishi katika mazingira mabaya. Ni sauti ya watoto wakitembea katikati ya mahema ya muda kwenye vichochoro vilivvyojubikwa na matope, hapa Gaza Kaskazini, huku wakijaribu kukwepa madimbwi ya maji yaliyosababishwa na mvua kubwa.Kupitia video iliyoandaliwa na UNICEF, Shahd Omar, msichana mwenye umri wa miaka kumi na saba, anaonekana amembeba nduguye, wengine wanaonekana wamekujikunyata kutokana na baridi. Shahd sasa akiwa amesimama nje hema lao anaelezea jinsi nyumba zao zilivyoharibiwa.“Tunavumilia hali ngumu sana,mvua kubwa, baridi, na upepo mkali, maisha ni magumu sana. Nyumba yetu ilivyoshambuliwa na kubomoka tulijitoa kwenye vif

  • Jifunze Kiswahili: Upatanisho wa kisarufi wa baadhi ya maneno

    20/02/2025 Duration: 52s

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili Mlumbi wa Lugha Joramu Nkumbi kutoka Tanzania anafafanua upatanisho wa kisarufi wa baadhi ya maneno kama vile "Ng'ombe kumi na minane ", vikombe viwili na mengineyo ambayo watu hutamka vibaya katika sentensi, mfano "Ng'ombe kumi na nane"

page 4 from 5