Habari Za Un
UNMISS yaimarisha doria jimboni Tambura Sudan Kusini
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:03:04
- More information
Informações:
Synopsis
Katika jitihada za kuimarisha amani na usalama katika maeneo yaliyoathiriwa na machafuko ya kikabila nchini Sudan Kusini, Umoja wa Mataifa kupitia Ujumbe wake wa amani nchini humo UNMISS wameendelea kuimarisha ulinzi na kuongeza doria za magari usiku na mchana huko Greater Tambura katika jimbo la Equatoria Magharibi.Sabrina Saidi anaangazia juhudi za UNMISS katika kuhakikisha hali ya usalama inarejea na wananchi waliokimbilia katika kambi za wakimbizi kusakama usalama wanarejea makwao.TAARIFA YA SABRINA SAIDI)NAT...Video ya UNMISS inaanza kwa kumulika doria zinazofanywa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko katika kaunti ya Greater Tambura katika jimbo la Western Equatoria, kusini-magharibi mwa nchi ya Sudan Kusini karibu na mipaka ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC na Jamuhuri ya Afrika ya Kati.Tangu mwaka 2021, mizozo ya wenyewe kwa wenyewe, umeendelea kugharimu maisha ya watu wengi na kuwalazimu maelfu kuyakimbia makazi yao.Wananchi waliokumbwa na hofu wamekuwa wakijificha vichakani, wengine