Habari Za Un
Wakimbizi Nyarugusu wahamasika kufanya usafi
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:02:40
- More information
Informações:
Synopsis
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa kushirikiana na Baraza la Wakimbizi la Norway NRC wanahakikisha wakimbizi wanaoishi katika kambi za wakimbizi za mkoani Kigoma Magharibi mwa Tanzania ikiwemo kambi ya nyarugusu wanapata huduma muhimu za maji na usafi kupitia ushirikiano wa viongozi wa wakimbizi. Huduma hizo zimekuwa changamoto kubwa katika kambi za wakimbizi zikichangiwa na ukata wa ufadhili. Flora Nducha na taarifa zaidi (TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipoibuka Burundi mwaka 2015, na baadaye mapigano kuighubika upya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, maelfu ya watu walikimbia na kuvuka mpaka kuingia Tanzania. Leo, wengi wao wanaishi katika kambi za wakimbizi mkoani Kigoma kama vile Mtendeli, Nduta, na Nyarugusu.Lakini maisha kambini hayajakuwa rahisi. Kwa ufadhili mdogo, familia zinapata shida kupata huduma za msingi kama maji safi, makazi, na elimu.Hapo ndipo Shirika la UNHCR, na Baraza la Wakimbizi la Norway NRC, wanapoingia. Tangu mwa