Habari Za Un

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 8:57:07
  • More information

Informações:

Synopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodes

  • 11 MACHI 2025

    11/03/2025 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea Mada kwa kina inayomulika mkutano wa CSW69 ulioanza Jana Jumatatu hapa New York, Marekani, ikiwa ni miaka 30 tangu mkutano wa nne wa kimataifa wa wanawake uliofanyika Beijing mwaka 1995, ukiweka msingi wa mabadiliko yanayoshuhudiwa sasa ya usawa wa kijinsia. Pia tunakuletea muhtasari na sauti za vijana kutoka mashinani.Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa asubuhi hii kwa saa za New York, Marekani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amekutana na wawakilishi wa Asasi za Kiraia wanaoshiriki Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake CSW69. Bwana Guterres amezitaka Asasi za Kiraia kuendelea kuzisukuma nchi kuweka mazingira bora kwa ajili ya usawa wa wanawake na wasichana na pia  akakumbushia kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuwaunga mkono katika kulitimiza lengo hilo.Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk kupitia Msemaji wake, ameripoti ukatili unaoendelea katika pwani ya Syria tangu Machi 6, ambapo anasema takriban raia 111 wameua

  • Ninataka kuwa dereva kama Fatuma Mfumia wa UNICEF nchini Tanzania

    10/03/2025 Duration: 02min

    Fatuma Mfumia ndiye dereva pekee wa kike katika shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF Tanzania. Fatuma ndiye tunayemwangazia leo. Video iliyorekodiwa na UNICEF Tanzania inamwonesha akiwa kwenye usukani, na hakika hapo utakubali anavyojiamini. Anold Kayanda na simulizi zaidi.

  • Mkutano wa CSW69 yang’oa nanga leo ikiwaleta pamoja washiriki zaidi ya 25,000

    10/03/2025 Duration: 03min

    Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani unaanza mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW69, kusanyiko kubwa zaidi la kila mwaka la Umoja wa Mataifa linalomulika usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake mwaka huu washiriki wakiwa zaidi ya 25,000. Selina Jeroboni na taarifa zaidi.

  • 10 MACHI 2025

    10/03/2025 Duration: 10min

    Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW69 na wakimbizi wanaokimbia machafuko nchini DRC kwenda Burundi. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani tunakupeleka nchini Lebanon, kulikoni?Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani unaanza mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW69, kusanyiko kubwa zaidi la kila mwaka la Umoja wa Mataifa linalomulika usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake mwaka huu washiriki wakiwa zaidi ya 25,000.Zaidi ya watu 63,000 sasa wamewasili Burundi wakikimbia machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na wengi wao wanaishi katika hali ngumu ndani ya uwanja wa michezo wa Rugombo jimboni Cibitoke (CHIBITOKE) huku wakisubiri kuhamishiwa kwenye kambi rasmi za wakimbizi.Makala leo tunamwangazia Fatuma Mfumia, dereva pekee wa kike katika shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhuduia Watoto, UNICEF Tanzania.Na mashina

  • UNHCR: Zaidi ya wakimbizi 63,000 wa DRC wamewasili Burundi wengi wanaishi kwenye uwanja wa Rugombo

    10/03/2025 Duration: 02min

    Zaidi ya watu 63,000 sasa wamewasili Burundi wakikimbia machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na wengi wao wanaishi katika hali ngumu ndani ya uwanja wa michezo wa Rugombo jimboni Cibitoke (CHIBITOKE) huku wakisubiri kuhamishiwa kwenye kambi rasmi za wakimbizi. Flora Nducha amefuatilia safari ya mmoja wa wakimbizi hao, kwako Flora.

  • Wanawake wajengewa uwezo wa tofauti ya matumizi ya lazima ni muhimu ili kujikwamua kiuchumi

    07/03/2025 Duration: 04min

    Mwaka 1995 huko Beijing, China kwenye mkutano wa nne wa kimataifa wa wanawake lilipitishwa Azimio la Beijing na Mpango wa Utekelezaji, ambalo pamoja na mambo mengine lililenga kusongesha haki za wanawake. Mwaka huu wa 2025 ikiwa ni miaka 30 baadaye, tathmini ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, inaonesha kuwa nchi zimesonga mbele katika usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake, kuanzia kuharamaisha ubaguzi kwenye ajira hadi mipango ya kuhimili tabianchi inayozingatia jinsia. Lakini bado kuna vikwazo vya kijamii, kiuchumi na kisiasa na ndio maana wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake mwaka huu wa 2025 kipaumbele ni kusongesha uwezeshaji, haki na usawa. Ni katika kumulika harakati hizo, Assumpta Massoi anakupeleka Singida nchini Tanzania kwenye maadhimisho yaliyoambatana na ujengeaji uwezo. 

  • UN: Sasa ni wakati wa kutimiza ahadi ya usawa wa kijinsia

    07/03/2025 Duration: 03min

    Katika kuelekea siku ya kimataifa ya wanawake ambayo huadhimishwa kila mwaka Machi 8 leo hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika hafla maalum ya kuadhimisha siku hiyo ambayo mwaka huu imebeba maudhui “Kwa wanawake na wasichana wote: haki, usawa, uwezeshaji.” Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women Sima Bahous amesema ni wakati wa kutekeleza kwa vitendo ndoto ya azimio la Beijing miaka 30 iliyopita la kufanya usawa wa kijinsi kuwa hali halisiKwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres pamoja na kupongeza mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kusongesha usawa wa kijinsia duniani amesemaNatts….“Hata hivyo, mafanikio haya yaliyopatikana kwa jitihada kubwa bado ni dhaifu na hayatoshi kabisa.Mateso ya muda mrefu, ukatili, ubaguzi na ukosefu wa usawa wa kiuchumi bado vinaathiri jamii zetu.Kila baada ya dakika kumi, mwanamke huuawa na mwenzi wake au mwanafamilia.”Ameongeza kuwa wanawake na wasichana milioni 612 wanai

  • 07 MACHI 2025

    07/03/2025 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake, na hali ya wanawake wajawaito nchini Ukraine. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani tunakupeleka nchini Kenya, kulikoni?Kuelekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake Machi 8, tathmini mpya ya Umoja wa Mataifa iliyowekwa wazi leo ikiangazia haki za wanawake miaka 30 baada ya Azimio la Beijing inaonesha uwepo wa maendeleo katika usawa wa kijinsia, kama vile sheria dhidi ya ubaguzi na sera jumuishi za kijinsia. Hata hivyo, ripoti hiyo inaeleza uwepo bado wa ubaguzi wa kijinsia uliojikita katika jamii, ukiendelea kuwazuia wanawake na wasichana kupata fursa.Zikiwa zimesalia siku mbili ya leo na kesho kufika tarehe 8 Machi Siku ya Kimataifa ya Wanawake, tunaendelea kuangazia hali ya wanawake duniani. Sharon Jebiichi anatupeleka Ukraine kutukutanisha na Mwakilishi wa muda wa Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu UNFPA nchini humo ambaye anaangazia madhila wanayokutana nayo wanawake wajawazito wa Ukraine.Katika makala Assumpta M

  • Ukraine: Mwakilishi wa UNFPA Ukraine Uller Muller na hali ya wanawake wajawazito nchini humo

    07/03/2025 Duration: 01min

    Zikiwa zimesalia siku mbili ya leo na kesho kufika tarehe 8 Machi Siku ya Kimataifa ya Wanawake, tunaendelea kuangazia hali ya wanawake duniani. Sharon Jebiichi anatupeleka Ukraine kutukutanisha na Mwakilishi wa muda wa Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu UNFPA nchini humo ambaye anaangazia madhila wanayokutana nayo wanawake wajawazito wa Ukraine.Ni Ulla Muller, Mwakilishi wa muda wa Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu UNFPA nchini Ukraine, akieleza kuhusu changamoto zinazowakumba wanawake wajawazito wa Ukraine.Anasema, “ninaweza kukuambia hadithi nyingi ambazo zimebaki nami kwa sababu nakutana na wanawake hawa kila mara, na mapenzi yangu kwao hayana mipaka.”Uller Muller anasimulia kisa cha mwanamke mmoja akisema,"Kuna mwanamke anayeitwa Ira ana umri wa miaka 31, na tayari anamlea mtoto mvulana wa umri wa miaka sita. Hivi karibuni aligundua kuwa ni mjamzito tena na anatarajia mapacha watatu. Ni hali ya kutisha na kuchanganya."Bi. Muller anaendelea kueleza kuwa mwanamke huyo aliku

  • Jifunze Kiswahili: Maana ya methali "Mchawi akifichua mirimo ya wachawi huuawa"

    06/03/2025 Duration: 01min

    Leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “MCHAWI AKIFICHUA MIRIMO YA WACHAWI HU UAWA”.

  • 06 MACHI 2025

    06/03/2025 Duration: 10min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Umoja wa Mataifa kupitia miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa Pamoja wa Kigoma, KJP nchini Tanzania, unaolenga kuhakikisha wanawake na wasichana wanajumuishwa kwenye mipango ya kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi, kwa kuwajengea uwezo.Kuelekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake Machi 8, tathmini mpya ya Umoja wa Mataifa iliyowekwa wazi leo ikiangazia haki za wanawake miaka 30 baada ya Azimio la Beijing inaonesha uwepo wa maendeleo katika usawa wa kijinsia, kama vile sheria dhidi ya ubaguzi na sera jumuishi za kijinsia. Hata hivyo, ripoti hiyo inaeleza uwepo bado wa ubaguzi wa kijinsia uliojikita katika jamii, ukiendelea kuwazuia wanawake na wasichana kupata fursa.Ripoti nyingine ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa leo ikiangazia Sudan imefichua vitendo vya watu kukamatwa kiholela, mateso, na unyanyasaji huko Khartoum vinavyotekelezwa na Vikosi vya wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) na pia Jeshi la Serikali ya Sudan (SAF). Ripoti hiyo imearifu pia kuwa m

  • Hali ya usalama ikidorora DRC, hofu sasa ni mustakabali wa watetezi wa haki za binadamu

    05/03/2025 Duration: 01min

    Hali ya kibinadamu ikiendelea kuzorota mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mtaalamu Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na hali ya watetezi wa haki za binadamu, Mary Lawlor leo ametoa wito wa msaada wa dharura na wa vitendo kwa watetezi wa haki za binadamu katika eneo hilo. Anold Kayanda na taarifa zaidi. (Taarifa ya Anold Kayanda)Mary Lawlor akizungumza leo jijini Geneva-Uswisi amesema, "watetezi wa haki za binadamu mashariki mwa DRC wako hatarini sana kulengwa na kulipiziwa kisasi kwa kazi yao ya kutetea haki za binadamu. Wanahitaji msaada sasa, ikiwa ni pamoja na usaidizi wa kuhamishwa kwa muda pamoja na familia zao.”Kundi la waasi la M23, limeendelea kusonga mbele katika eneo hilo la mashariki mwa DRC tangu lilipoanza mashambulizi yake mapema mwaka huu, na wale waliorekodi na kufichua ukiukwaji wa haki zao wamekuwa wakilengwa moja kwa moja, amesisitiza Bi. Lawlor."Katika wiki za hivi karibuni nimepokea taarifa nyingi za tahadhari zinazohitaji msaada na nimezungumza moja kwa moja

  • Miaka 30 baada ya Azimio la Beijing kuhusu haki za wanawake, safari bado ni ndefu

    05/03/2025 Duration: 02min

    Kuelekea siku ya wanawake duniani itakayoadhimishwa mwishoni mwa wiki hii ambayo ni tarehe 8 mwezi Machi, Mkurugenzi Mtendaji wa  shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women, Sima Bahous, amesisitiza kwamba ahadi zilizowekwa kwenye Azimio la Beijing miaka 30 iliyopita kuhusu haki za wanawake hazipaswi tu kukumbukwa bali zinahitaji kutekelezwa kikamilifu. Flora Nducha anafafanua zaidiAkizungumza wiki hii mjini Geneva Uswisi katika majadiliano ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ya kuadhimisha miaka 30 ya Azimio la Beijing (#Beijing30), Bi. Bahous amebainisha umuhimu wa kuharakisha maendeleo ya usawa wa kijinsia akiwataka viongozi wa dunia kuchukua hatua thabiti ili kuhakikisha haki za wanawake zinapewa kipaumbele wakati wa changamoto zinazoendelea duniani.Amesema “Miaka 30 iliyopita dunia iliweka ahadi ya kusongesha fursa na utu wa wanawake na wasichana wote. Ahadi hiyo haikuwa maneno matupu kwenye karatasi, ilikuwa ramani ya njia na wito wa mshikamano . Na kwa

  • 05 MACHI 2025

    05/03/2025 Duration: 09min

    Hii leo jarida linamulika wasiwasi kuhusu hali ya watetezi wa haki za binadamu nchini DRC, wakati huu hali ya usalama si shwari mashariki mwa nchi; kuelekea siku ya wanawake duniani, Mkuu wa UN Women arejelea Azimio la Beijing; vilabu vya Dimitra  nchini DRC vinavyosaidia wanawake na wanaume kuketi pamoja na kutatua changamoto zinazowakabilia; mashinani ni Ramadhani huko Gaza.Hali ya kibinadamu ikiendelea kuzorota mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mtaalamu Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na hali ya watetezi wa haki za binadamu, Mary Lawlor leo ametoa wito wa msaada wa dharura na wa vitendo kwa watetezi wa haki za binadamu katika eneo hilo. Anold Kayanda na taarifa zaidi.Kuelekea siku ya wanawake duniani itakayoadhimishwa mwishoni mwa wiki hii ambayo ni tarehe 8 mwezi Machi, Mkurugenzi Mtendaji wa  shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women, Sima Bahous, amesisitiza kwamba ahadi zilizowekwa kwenye Azimio la Beijing miaka 30 iliyopita kuhusu haki za wanawak

  • Vilabu vya Dimitra vyaimarisha usawa wa kijinsia na uchumi DRC

    05/03/2025 Duration: 04min

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO limesaidia kujenga utangamano wa kijamii kwa kuboresha maisha kwenye eneo la Walungu jimboni Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Limefanya hivyo kupitia vilabu vya Dimitra ambavyo hupatia wanawake, wanaume na vijana fursa ya uongozi wa kuleta mabadiliko chanya kwa kutatua changamoto zilizo kwenye jamii yao bila hata kuwa tegemezi kwa msaada wa nje. Mradi huu ulitekelezwa kati ya mwaka 2008 na 2023 na sasa tunamulika ni kwa vipi umeleta mafanikio. Sharon Jebichii anaelezea kwenye makala hii kupitia video iliyoandaliwa na FAO. 

  • 04 MACHI 2025

    04/03/2025 Duration: 10min

    Kituo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani Tanzania (TPTC) kilichoko chini ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ/TPDF) kinavyotumia  sanaa ya muziki kuelimisha walinda amani kuhusu ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa kingono. Makala hii iliyokusanywa na Florean Kiiza wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania kwa kushirikiana na Kapteni Mwijage Francis Inyoma wa JWTZ imechakatwa na Anold Kayanda na inasimuliwa na Flora Nducha.

  • Napenda sana maabara na imenihamasisha kusoma sayansi - Zamzam

    03/03/2025 Duration: 02min

    Nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na wadau wengine wanafanikisha mpango wa kuhamasisha wasichana kuingia katika masomo ya STEM yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati. Baadhi ya wasichana wakimbizi katika kambi ya Dadaab nchini Kenya ni wanufaika wa mpango huu. Sharon Jebiichi na maelezo zaidi.Zamzam Hussein,aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Hagadera. Ni mkimbizi mwenye asili ya Somalia na sasa anaishi katika kambi ya wakimbizi ya Daadab nchini Kenya akiwa na ndoto ya kuwa daktari. Kupitia mpango huu ambao ni sehemu ya programu ya PROSPECTS ambao ni ushirikiano wa kimataifa unaojumuisha mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa ukilenga kuboresha upatikanaji wa elimu, ulinzi wa jamii, na ajira yenye hadhi kwa jamii zinazowakaribisha wakimbizi na watu waliolazimika kuhama makazi yao Zamzam Hussein ameweza kukumbatia sayansi.“Nilikuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Hagadera na nikamaliza elimu yangu mwaka wa 2024. Nilijiunga na shule hiyo Agosti 2021

  • Viongozi wababe, wa kiimla na wenye fedha wanasigina haki za binadamu duniani

    03/03/2025 Duration: 02min

    Kwenye kikao cha 58 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kinachoendellea mjini Geneva Uswisi, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa M ataifa, Volker Türk , amezungumzia hali ya kuzorota na kutoeleweka inayohusu haki za binadamu duniani kote akielezea wasiwasi mkubwa kuhusu kudhoofika kwa makubaliano ya kimataifa kuhusu haki za binadamu,na kuonya kwamba ushawishi wa viongozi wa kiimla, matajiri wakubwa, na viongozi wa kimabavu unatishia kuvuruga maendeleo ya miongo kadhaa. Anold Kakayanda na taarifa kamili.Asante Flora katika taarifa yake Türk  amesisitiza umuhimu wa kuhifadhi haki za binadamu na utawala wa sheria ili kuzuia kurudiwa kwa ukatili wa zamani.Moja ya masuala ya dharura yaliyotiliwa mkazo na Türk  ni mgogoro wa kibinadamu unhaoendelea huko Gaza. Amelaani uharibifu uliosababishwa na hatua za kijeshi za Israeli dhidi ya mashambulizi ya Oktoba 7, 2023 yaliyofanywa na Hamas na makundi mengine ya wapiganaji wa Kipalestina.Türk  amesisitiza haja ya kudumisha usit

  • Burundi yahamishia wakimbizi wa DRC eneo salama zaidi

    03/03/2025 Duration: 03min

    Machafuko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) yanaendelea kufurusha watu na wengine wanaamua kukimbilia nchi jirani ikiwemo Burundi. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini Burundi limesema wazi kuwa katika wiki mbili za mwezi Februari kuanzia tarehe 14 walipokea wakimbizi zaidi ya 60,000, wengi wakiwa tayari walishafurushwa awali. Kwa waliowasili katika eneo la Kaburantwa  nchini Burundi, bado wanahofia usalama. Serikali ya Burundi imetenga eneo lingine salama zaidi na sasa wanahamishiwa huko. Je ni wapi? Assumpta Massoi kwa msaada wa video ya UNHCR Burundi anasimulia zaidi. 

  • 03 MACHI 2025

    03/03/2025 Duration: 11min

    Karibu jaridani hii leo na mwenyeji wako ni Flora Nducha akikuletea habari kuhusu haki za binadamu, elimu ya STEM kwa wasichana wakimbizi nchini Kenya; Harakati za kuhamishia wakimbizi wa DRC nchini Burundi kuelekea maeneo salama; mafunzo ya ujasiriamali wa ushoni kwa wanawake na wasichana.Kwenye mkutano wa 58 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu unaoendelea mjini Geneva Uswisi, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu  Volker Türk , amezungumzia hali ya kuzorota na kutoeleweka inayohusu haki za binadamu duniani, akionya kwamba ushawishi wa viongozi wa kiimla, matajiri wakubwa, na viongozi wa kimabavu unatishia kuvuruga maendeleo ya miongo kadhaa. Ripoti yake Anold Kayanda.Nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na wadau wengine wanafanikisha mpango wa kuhamasisha wasichana kuingia katika masomo ya STEM yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati.Ripoti yake Sharon Jebiichi.Makala Assumpta Massoi anakupeleka mpakani mwa Burundi na Jamhuri ya Ki

page 3 from 5