Habari Za Un

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 8:57:07
  • More information

Informações:

Synopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodes

  • 20 MACHI 2025

    20/03/2025 Duration: 12min

    Hii leo jaridani katika mada kwa kina tunajikita katika mkutano CSW69 ambao umebakiza siku moja tu, kesho Machi 21 unakunja jamvi, na tunamsikia Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Tanzania, Waziri Riziki Pembe kutoka Zanzibar na Profesa Smile Dzisi, Mkugenzi wa Shirika la “I believe Global” kutoka Ghana.Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi amesema kukata ufadhili kwa mashirika yanayotoa huduma za kibinadamu kunasababisha janga la uwajibikaji. Kupitia taarifa iliyotolewa leo Geneva, Uswisi na UNHCR, Bwana Grandi amesema kukata ufadhili kunaweka hatarini maisha ya mamilioni ya watu na madhara yake kwa watu wanaokimbia majanga, yatakuwa makubwa zaidi na yataonekana wazi ikiwemo wanawake na watoto wa kike kukosa huduma zitokanazo na kubakwa.Leo ni siku ya furaha duniani maudhui yakimulika umuhimu wa watu kusaidiana na kujaliana katika masuala mbalimbali ikiwemo chakula. Ripoti mpya ya wadau wa UN iliyozinduliwa leo imeonesha kuwa nchi ye

  • Lengo langu ni kuona wasichana wadogo wanashiriki kwa wingi CSW - Zahra Salehe ICCAO

    19/03/2025 Duration: 03min

    Katika makala Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anazungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ICCAO kutoka Tanzania, Zahra Salehe, mshiriki mwingine kutoka Tanzania anayehudhuria mkutano wa 69 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW69 unaoendelea hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, jijini New York Marekani. 

  • Haki za wanawake na wasichana lazima zizingatiwe na zipewe kipaumbele - Ochieng CSW69

    19/03/2025 Duration: 02min

    Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 unaendelea kujadili mafanikio yaliyopatikana na nini kifanyike zaidi kutimiza lengo la miaka 30 iliyopita la azimio la Beijing. Mwanzilishi na mkurugenzi mkuu wa shirika la slums foundation lililoko  jijiniNairobi, Kenya naye anashiriki mkutano huu wa CSW69 na ameueleza Sharon Jebichii wa Idhaa hii  kilichomleta hapa, matarajio yake na ushauri kwa wasichana na wanawake.

  • 19 NACHI 2025

    19/03/2025 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na binadamu, na yaliyojiri hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa mkutano wa 69 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW69.Madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na binadamu yameongezeka kwa viwango vya kutisha mwaka 2024, na baadhi ya athari hasi zinaweza kuwa zisizoweza kurekebishwa kwa karne nyingi – kama si milenia, imesema ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, (WMO).Tukirejea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 unaendelea kujadili mafanikio yaliyopatikana na nini kifanyike zaidi kutimiza lengo la miaka 30 iliyopita la azimio la Beijing. Mwanzilishi na mkurugenzi mkuu wa shirika la slums foundation lililoko  jijiniNairobi, Kenya naye anashiriki mkutano huu wa CSW69 na ameueleza Sharon Jebichii wa Idhaa hii  kilichomleta hapa, matarajio yake na ushauri kwa wasichana na wanawake..Makala Flora Nducha wa Idhaa hii anazun

  • WMO: Joto likizidi kuongezeka duniani, mwaka 2024 wathibitishwa kuwa ulikuwa wa joto zaidi

    19/03/2025 Duration: 01min

    Madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na binadamu yameongezeka kwa viwango vya kutisha mwaka 2024, na baadhi ya athari hasi zinaweza kuwa zisizoweza kurekebishwa kwa karne nyingi – kama si milenia, imesema ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, (WMO). Anold Kayanda na maelezo zaidi.

  • 18 MACHI 2025

    18/03/2025 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumulika elimu ya mtoto wa kike kama moja ya nguzo muhimu katika jamii ukizingatia malengo endelevu ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa.Pia tunakuletea muhtasari wa habari na sauti za mashinani.Viongozi wa Umoja wa Mataifa leo wamelaani vikali mashambulizi ya anga ya Israel huko Ukanda wa Gaza na kutoa wito kwa kusitisha uhasama mara moja. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonesha mshtuko na wasiwasi mkubwa kuhusu mashambulizi hayo akitoa wito kwa pande zote kuheshimu usitishaji mapigano, kurejesha misaada ya kibinadamu bila vikwazo, na kuhakikisha kuachiliwa mara moja na bila masharti kwa mateka waliobaki.Ghasia zinazoendelea katika kaunti za Nasir, Ulang, na Baliet, Jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini zimeathiri vibaya jamii za eneo hilo na shughuli za kibinadamu, na kusababisha watu takriban 50,000 kukimbia makazi yao tangu mwishoni mwa mwezi Februari amesema Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini S

  • Melvin Wajir: Ushiriki wa wanawake unapaswa kuwa mezani na sio katika menyu

    17/03/2025 Duration: 03min

    Ili kufanikisha lengo la usawa wa kijinsia Umoja wa Mataifa unasisitiza ushiriki wa wanaume katika mchakato hasa kwa kuzingatia kuwa mfumo dume miaka nenda miaka rudi umekuwa kikwazo cha kufikia lengo hilo, Flora Nducha wa idhaa hii amebahatika  kuzungumza na mmoja wa wanaume wanaoshiriki mkutano huo kusikia maoni yake.

  • UNCTAD: Wekeni wazi mikataba ya madeni mnayokopa ili kujenga imani kwa wananchi

    17/03/2025 Duration: 01min

    Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Usimamizi wa madeni umeanza rasmi hii leo huko Geneva Uswisi ambapo kubwa linalojadiliwa ni namna ya kuhakikisha wakati serikali zikipambana kulipa madeni hazidumazi maendeleo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Assumpta Massoi

  • 17 MACHI 2025

    17/03/2025 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia madeni katika nchi zenye mapato ya chini na ujumbe wa washiriki wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani CSW69 hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa.Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Usimamizi wa madeni umeanza rasmi hii leo huko Geneva Uswisi ambapo kubwa linalojadiliwa ni namna ya kuhakikisha wakati serikali zikipambana kulipa madeni hazidumazi maendeleo.Akijibu swali la kwa nini pamoja na ongezeko na idadi ya wanawake katika ngazi za uamuzi nchini Tanzania lakini bado kuna changamoto zinazoukabili usawa wa kijinsia, Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu anayehudhuria mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake, CSW69 jijini New York, Marekani kupitia mahojiano maalumu na Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa, anaeleza kuwa      mabadiliko chanya katika jamii hayaji kwa kutumia mabavu.Makala pia inatubakisha hapa Umoja wa Mataifa kwenye mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani CSW69.

  • Mabadiliko chanya katika jamii yanakuja kwa kueleweshana - Dkt. Gwajima

    17/03/2025 Duration: 02min

    Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Waziri, Dkt. Dorothy Gwajima,  ni mmoja wa wanaohudhuria mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake, CSW69 hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Anold Kayanda wa Idhaa hii amekutana naye na miongoni mwa mambo mengi amemuuliza ni kwa nini pamoja na ongezeko na idadi ya wanawake katika ngazi za uamuzi nchini Tanzania lakini bado kuna changamoto nyingi zinazoukabili usawa wa kijinsia nchini humo?

  • Azimio la Beijing limeleta manufaa kwa wanawake Côte d'Ivoire - Francine

    14/03/2025 Duration: 04min

    Kutana na Francine Aka Epse Akaanghui  Rais wa Chama cha wanasheria wanawake nchini Côte d'Ivoire huko Afrika Magharibi. Yeye anashiriki mkutano wa 69 wa Hali ya Wanawake duniani, CSW69 akisema taifa lake lina mengi ya kujivunia wakati huu wa kuadhimisha miaka 30 tangu kupitishwa kwa Azimio la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji. Francine amezungumza na Assumpta Massoi katika makala hii.

  • 14 MACHI 2025

    14/03/2025 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres huko Bangladesh, na yaliyojiri hapa makao makuu katika mkutano wa CSW69. Makala na mashinani tunasalia hapa hapa makao makuu, kulikoni?Akiwa ziarani katika kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani, Cox’s Bazar, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo Machi 14 ameonya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayowakabili zaidi ya wakimbizi milioni moja wa Rohingya nchini Bangladesh.Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 unaendelea kujadili mafanikio yaliyopatikana na nini kifanyike zaidi kutimiza lengo la miaka 30 iliyopita la azimio la Beijing. Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano huo wa mwaka 1995 yuko kwenye mkutano huu CSW69 Flora Nducha wa Idhaa alipata fursa ya kuuliza nini tathimini yake ya utekelezaji wa azimio la Beijing na kinachohitajika zaidi kutimiza lengo la azimio hilo.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC hii leo Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda ama

  • Katibu Mkuu afuturu na wakimbizi wa Rohingya nchini Bangladesh

    14/03/2025 Duration: 01min

    Leo Ijumaa ikiwa ni siku ya 11 ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amefuturu na wakimbizi wa Rohingya walioko  kwenye kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani, Cox Baazar nchini Bangladesh kuonesha mshikamano na wakimbizi na wenyeji wanaowahifadhi. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

  • Getrude Mongella: Ukilinganisha na tulikotoka tumepiga hatua lakini safari bad oni ndefu

    14/03/2025 Duration: 01min

    Tukirejea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 unaendelea kujadili mafanikio yaliyopatikana na nini kifanyike zaidi kutimiza lengo la miaka 30 iliyopita la azimio la Beijing. Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano huo wa mwaka 1995 yuko kwenye mkutano huu CSW69 Flora Nducha wa Idhaa alipata fursa ya kuuliza nini  tathimini yake ya utekelezaji wa azimio la Beijing na kinachohitajika zaidi kutimiza lengo la azimio hilo. 

  • Jifunze Kiswahili: Maana ya neno Wakfu

    13/03/2025 Duration: 01min

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchambuzi wetu Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua neno Wakfu.

  • 13 MACHI 2025

    13/03/2025 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo Idhaa hii imezungumza na Lucy Gidamis, Wakili ambaye kwa sasa anafanya kazi na shirika la Msichana Initiative nchini Tanzania akijikita katika kutetea na kutekeleza haki za wanawake. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa neno Wakfu.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC hii leo Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO umekabidhi magari sita kwa gavana wa kijeshi wa jimbo la Kivu Kaskazini ili kuwezesha shughuli za polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama.Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Afya duniani WHO na la kuhudumia watoto UNICEF yametangaza kuwepo kwa idadi kubwa ya wagonjwa wa surua barani ulaya, jumla ya wagonjwa 127,350 waliripotiwa kati yao watoto wakiwa zaidi ya asilimia 40.Na hii leo ikiwa ni chungu cha 10 cha Ramadhan, ikikamilisha fungu la kwanza kati ya mafungu matatu ambapo ni siku 30 za mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameanza ziara yake ya siku nne nchini B

  • Haki Elimu - Ujumbe wetu mkuu kwenye CSW69 ni elimu kwa mtoto wa kike

    12/03/2025 Duration: 03min

    Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, (CSW69) umeingia siku ya tatu hii leo Machi 12 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijinoi New York, Marekani. Mkutano huu wa mwaka huu unafanyika katika hali ya kihistoria kwa kuzingatia kuwa ni miaka 30 tangu Mkutano wa wanawake ulipofanyika jijini Beijing - China  mwaka 1995 na kuweka maazimio muhimu kuhusu masuala mazito ya kumkomboa mwanamke dhidi ya ukandamizaji kote duniani. Maelfu ya wanawake na wadau wengine wanakutana kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York. Miongoni mwao ni Nuria Mshare ambaye amewakilisha taasisi ya Haki Elimu ya nchini Tanzania.

  • 12 MACHI 2025

    12/03/2025 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia mpango mpya wa UN80, unaolenga kuimarisha kazi na ufanisi wa chombo hicho ambacho mwaka huu kinatimiza miaka 80, na yaliyojiri katika mkutano wa CSW69. Makala na mashinani tunasalia hapa hapa makao makuu, kulikoni?Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amezindua Mpango mpya wa UN80, unaolenga kuimarisha kazi na ufanisi wa chombo hicho ambacho mwaka huu kinatimiza miaka 80 tangu kuanzishwa kwake huku akisisitiza umuhimu wa mshikamano wa kimataifa..Wakati mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 ukiendelea hapa New York Marekani nchini Sudan Kusini wanawake na wasichana wanaendelea kuonja shubiri ya vita, wakibakwa, kuuawa, kukosa elimu na kupitia changamoto nyingine lukuki sababu ya vita. Mmoja wa washiriki wa mkutano wa CSW69 kutoka Sudan Kusini akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili amesema sasa imetosha amekuja na ujumbe mmoja tu, anataka jinamizi la vita lazima likome.Makala tukisalia hapa hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataif

  • Jumuiya ya kimataifa ishikeni mkono Sudan Kusini kwa maslahi ya wananchi - Micklina Kenyi

    12/03/2025 Duration: 02min

    Wakati mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 ukiendelea hapa New York Marekani nchini Sudan Kusini wanawake na wasichana wanaendelea kuonja shubiri ya vita, wakibakwa, kuuawa, kukosa elimu na kupitia changamoto nyingine lukuki sababu ya vita. Mmoja wa washiriki wa mkutano wa CSW69 kutoka Sudan Kusini akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili amesema sasa imetosha amekuja na ujumbe mmoja tu, anataka jinamizi la vita lazima likome. 

  • Katibu Mkuu azindua Mpango wa kuchechemua utendaji wa shirika

    12/03/2025 Duration: 02min

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amezindua Mpango mpya wa UN80, unaolenga kuimarisha kazi na ufanisi wa chombo hicho ambacho mwaka huu kinatimiza miaka 80 tangu kuanzishwa kwake huku akisisitiza umuhimu wa mshikamano wa kimataifa. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

page 2 from 5