Habari Za Un
UN yatumia kila mbinu kuhakikisha inawafikia waathirika wa tetemeko Afghanistan
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:02:22
- More information
Informações:
Synopsis
Juhudi kubwa za msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililoipiga Afghanstan mwishoni mwa wiki, zimeendelea leo huku watoa misaada wakikabiliwa hali ngumu ya kuwafikia wanaohitaji msaada kutokana na Barabara kuzibwa na kukatika kwa mawasiliano. Anold Kayanda na taarifa zaidi.(Taarifa ya Anold Kayanda)Taarifa mpya kutoka kwa timu za tathmini za Umoja wa Mataifa zilizofanikiwa kuwafikia waathirika katika wilaya ya milimani ya Ghazi Abad jana Jumanne kwa njia ya miguu, zimeweka wazi umuhimu wa kuendeleza tena kwa haraka msaada wa kibinadamu.Salam Al-Jabani kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) mjini Kabul anasema, “jambo la dharura ni kuwatoa watu chini ya vifusi na Watu wanasema wanachohitaji kwa haraka ni msaada wa kuwazika waliofariki dunia na kuwatoa waliofunikwa.”UNICEF inasema watoa misaada wake walilazimika kutembea kwa saa mbili ili kuwafikia watu na bado kuna vijiji ambavyo ili kuvifikia unahitaji kutumia saa sita hadi saba na hata helikopta hazijafanikiwa kufika huko