Habari Za Un

28 OKTOBA 2024

Informações:

Synopsis

Hii leo jaridani tunaangazia janga la nja linalokumba wananchi waathirika wa mizozo nchini Sudan, na simulizi za walinda amani wa UNIFIL nchini Lebanon. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Haiti, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) leo kwa mara nyingine tena limetahadharisha kwamba bila msaada wa kibinadamu nchini Sudan, mamia ya maelfu wanaweza kufa kwa njaa.Kikosi cha muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, UNIFIL, ambapo, katikati ya mvutano unaoongezeka kati ya Lebanon na Israel, walinda amani walioko katika makao makuu ya UNIFIL huko Naqoura wamekuwa wakivumilia mazingira magumu. Ushuhuda wa hivi karibuni kutoka kwa walinda amani hao unaonesha ukubwa wa changamoto wanazokabiliana nazo, ikiwemo vitisho vilivyoongezeka kutoka kwa shughuli za kijeshi za Israel zilizo karibu na eneo hilo, vizuizi vya kusafiri, na changamoto za uendeshaji wa shughuli.Makala inatupeleka Nairobi Kenya kwa washindi waliotwaa tuzo ya “Mtu Bora wa Mwaka wa Umoja wa Mataifa 20