Habari Za Un

UN: Hali si hali tena Gaza vifo vyatawala hospitali na kwa raia hata mkate ni adimu kupatikana

Informações:

Synopsis

Hali Gaza inaendelea kuwa tete wakati ucheleweshwji wa kuhamisha wagonjwa hususan watoto wanaohitaji msaada wa haraka wa huduma za afya imekuwa ni hukumu ya kifo kwao huku maelfu ya watu wakiendelea kukosa mahitaji ya muhimu ya kila siku ikiwemo chakula kama mkate, yameonya leo mashirika ya Umoja wa Mataifa.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeonya kwamba idadi ya watoto wanaohamishwa Gaza kwa ajili ya huduma za dharura za matibabu imeshuka sana hadi kufikia mtoto mmoja kwa siku na kusema kiwango hiki kikiendelea itachukua zaidi ya miaka 7 kuhamisha watoto 2500 wanaohitaji huduma ya dharura ya matibabu.Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis msemaji wa UNICEF James Elder amesema “matokeo yake watoto wanakufa Gaza sio tu kutokana na mabomu na risasi na makombora yanayofurusmishwa lakini kwa sababu hata kama miujiza inatokea , hata kama mabomu yanalipuka na nyumba kuporomoka, na vifo kuongezeka watoto wananusurika, lakini kisha wanazuiliwa kuondoka Gaza Kwenda kupokea huduma