Habari Za Un
13 FEBRUARI 2025
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:11:05
- More information
Informações:
Synopsis
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulika siku ya redio duniani, maudhui yakiwa Radio na Tabianchi, na ni kwa vipi chombo kinachodaiwa kutwamishwa na maendeleo ya teknolojia kinaendelea kusaidia kuelimisha umma kuhusu madhara ya mabadiliko ya tabianchi, Teonas Aswile wa TBC Taifa nchini Tanzania anaeleza.Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambapo hali inazidi kuwa tete na leo Mkurugenzi Mtendaji wa shirkika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, Catherine Russell, ameelezea wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa ghasia mashariki mwa mwa nchi hiyo katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, ambapo watoto na familia wanakabiliwa na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.Naibu mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masiala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA nchini Sudan Edmore Tondhlana akizungumza na UN News amesema hali nchini Sudan inaendelea kuwa janga la kibinadamu wakati vita ikishika kasi na watu wakiendelea kufurushwa makwao. Amesema "