Habari Za Un

Akibomoa kibanda chake Goma DRC, mkimbizi asema ana hofu kurejea Saké

Informações:

Synopsis

Baada ya waasi wa M23 jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupatia wakimbizi waliokuwa wamesaka hifadhi kambini mjini Goma, wawe wamerejea makwao ndani ya saa 72 kuanzia juzi jumatatu, mamia wameanza kutii amri hiyo.Miongoni mwao ni Kibira Bakulu, baba wa watoto 5, aliyekimbia mapigano eneo la Saké, mwezi Februari mwaka jana, takriban kilomita 10 kutoka Goma.Akiwa katika harakati za kubomoa kibanda chake katika kambi ya nane ya CEPAC Mugunga huko Goma, Bwana Bakulu anasema walishangaa, bila kuwa tayari, kuambiwa warudi walikotoka."Tumepatiwa saa 72 tuwe tumeondoka na kurejea Saké, kwani vita vimeisha. Sisi hatua uhakika kamili kwa sababu tuliondoka Saké kutokana na vita. Kama inabidi kusukumwa tuondoke, hatuna la kuchagua,” amesema Bwana Bakulu.Ana hofu ya kurejea Saké, akisema, “kule tulikuwa tunaishi Sake na tukirejea tutaishi vipi? Tunaomba viongozi wajitahidi watusaidie ili watuhakikishia usalama.Alipoeleza hali halisi amesema, “ hii siku ya leo hapa unaniona, watu w