Habari Za Un

12 FEBRUARI 2025

Informações:

Synopsis

Hii leo jaridani tunaangazia matokeo ya maandamani nchini Bangladesh, na machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala inatupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi na ofisi ya haki za binadamu (OHCHR) imefichua kuwa viongozi wa juu wa serikali ya Bangladesh walihusika moja kwa moja katika ukandamizaji wa maandamano makubwa yaliyoitikisa nchi hiyo mwaka 2024 na kusababisha vifo vingi.Baada ya waasi wa M23 jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupatia wakimbizi waliokuwa wamesaka hifadhi kambini mjini Goma, wawe wamerejea makwao ndani ya saa 72 kuanzia juzi jumatatu, mamia wameanza kutii amri hiyo licha ya hofu inayowakabili ya kule wanakotakiwa kurejea.Makala inatupeleka jijini Nairobi, Kenya ambako ambako Kevin Keitany wa redio washirika wetu Domus FM kwa kuzingatia kuwa kesho Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio, ametutumia maoni ya vijana wawili wanaozungumzia namna r