Habari Za Un
28 FEBRUARI 2025
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:11:19
- More information
Informações:
Synopsis
Hii leo jaridani tunaangazia migogoro ambayo yameendelee kwa muda mrefu Sudan Kusini, na ujumbe wa Katibu Mkuu ikielekea kuanza kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Makala inatupeleka nchini Kenya, na mashinani nchini Tanzania.Viongozi wa kisiasa wa Sudan Kusini lazima wakabiliane na ukwepaji wa sheria na ufisadi unaochochea ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, la sivyo watahatarisha mpito wa kisiasa wa nchi hiyo, imesema Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Sudan Kusini katika ripoti yake iliyotolewa leo.Kuelekea kuanza kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwishoni mwa wiki hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma ujumbe wake wa kutaka kipindi hicho cha takribani siku 30 kitumike kuleta amani na kuongoza kuelekea dunia yenye yenye haki na huruma zaidi..Katika makala Anold Kayanda wa Idhaa hii kutokana na video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, anakupeleka nchini Kenya kukutanisha na mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC am