Habari Za Un
UNICEF na WFP wawezesha watoto nchini Sudan Kusini kwenda shule ili watimize ndoto zao
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:02:03
- More information
Informações:
Synopsis
Mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la Kuhudumia Watoto, UNICEF na la Mpango wa Chakula duniani, WFP kwa kushirikiana na mradi wa pamoja wa kimataifa wa mnepo ,au Joint Resilience Project (JRP) nchini Sudan Kusini ,wanatekeleza msaada wa chakula bora na salama bila malipo kwa watoto shuleni ,kwa zaidi ya wanufaika laki tano alfu Hamsini 550,000 ili kuhakikisha ndoto za watoto hao zinatimia. Ni sauti ya watoto wakitembea kuelekea shuleni huku wakiwa wamevibeba vitabu vyao mikononi.Kupitia video iliyoandaliwa na UNICEF, Tieng Maleng, mnufaika wa mradi wa JRP kutoka kijiji cha Pangapdit anaonekana akiwapa watoto wake kiamsha kinywa huku wakiwa wamekaa nje ya boma lao wakiwa wamevalia sare zao tayari kwenda shule. Kwa furaha anaeleza jinsi mradi huu umekuwa wa manufaa kwa familia yake.“Baada ya kupokea msaada wa kifedha, nilitumia fedha kidogo kulipa ada ya shule ya watoto wangu. Nikachukua sehemu kidogo ya fedha hizo kununua viatu vyao, na dawa. Pia nilitumia sehemu nyingine ya msaada huo katika kilimo