Habari Za Un
Hali ya usalama ikidorora DRC, hofu sasa ni mustakabali wa watetezi wa haki za binadamu
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:01:57
- More information
Informações:
Synopsis
Hali ya kibinadamu ikiendelea kuzorota mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mtaalamu Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na hali ya watetezi wa haki za binadamu, Mary Lawlor leo ametoa wito wa msaada wa dharura na wa vitendo kwa watetezi wa haki za binadamu katika eneo hilo. Anold Kayanda na taarifa zaidi. (Taarifa ya Anold Kayanda)Mary Lawlor akizungumza leo jijini Geneva-Uswisi amesema, "watetezi wa haki za binadamu mashariki mwa DRC wako hatarini sana kulengwa na kulipiziwa kisasi kwa kazi yao ya kutetea haki za binadamu. Wanahitaji msaada sasa, ikiwa ni pamoja na usaidizi wa kuhamishwa kwa muda pamoja na familia zao.”Kundi la waasi la M23, limeendelea kusonga mbele katika eneo hilo la mashariki mwa DRC tangu lilipoanza mashambulizi yake mapema mwaka huu, na wale waliorekodi na kufichua ukiukwaji wa haki zao wamekuwa wakilengwa moja kwa moja, amesisitiza Bi. Lawlor."Katika wiki za hivi karibuni nimepokea taarifa nyingi za tahadhari zinazohitaji msaada na nimezungumza moja kwa moja