Habari Za Un
05 MACHI 2025
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:09:58
- More information
Informações:
Synopsis
Hii leo jarida linamulika wasiwasi kuhusu hali ya watetezi wa haki za binadamu nchini DRC, wakati huu hali ya usalama si shwari mashariki mwa nchi; kuelekea siku ya wanawake duniani, Mkuu wa UN Women arejelea Azimio la Beijing; vilabu vya Dimitra nchini DRC vinavyosaidia wanawake na wanaume kuketi pamoja na kutatua changamoto zinazowakabilia; mashinani ni Ramadhani huko Gaza.Hali ya kibinadamu ikiendelea kuzorota mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mtaalamu Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na hali ya watetezi wa haki za binadamu, Mary Lawlor leo ametoa wito wa msaada wa dharura na wa vitendo kwa watetezi wa haki za binadamu katika eneo hilo. Anold Kayanda na taarifa zaidi.Kuelekea siku ya wanawake duniani itakayoadhimishwa mwishoni mwa wiki hii ambayo ni tarehe 8 mwezi Machi, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women, Sima Bahous, amesisitiza kwamba ahadi zilizowekwa kwenye Azimio la Beijing miaka 30 iliyopita kuhusu haki za wanawak