Habari Za Un
17 MACHI 2025
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:11:28
- More information
Informações:
Synopsis
Hii leo jaridani tunaangazia madeni katika nchi zenye mapato ya chini na ujumbe wa washiriki wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani CSW69 hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa.Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Usimamizi wa madeni umeanza rasmi hii leo huko Geneva Uswisi ambapo kubwa linalojadiliwa ni namna ya kuhakikisha wakati serikali zikipambana kulipa madeni hazidumazi maendeleo.Akijibu swali la kwa nini pamoja na ongezeko na idadi ya wanawake katika ngazi za uamuzi nchini Tanzania lakini bado kuna changamoto zinazoukabili usawa wa kijinsia, Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu anayehudhuria mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake, CSW69 jijini New York, Marekani kupitia mahojiano maalumu na Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa, anaeleza kuwa mabadiliko chanya katika jamii hayaji kwa kutumia mabavu.Makala pia inatubakisha hapa Umoja wa Mataifa kwenye mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani CSW69.