Habari Za Un
Wanawake wamefanya mengi lakini hayajarekodiwa - Dkt. Reuben CSW69
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:03:50
- More information
Informações:
Synopsis
Rekodi ni chache sana ya vitu ambavyo wanawake wamefanya hapa duniani, anasema Dkt. Rose Reuben, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania anapozungumza na Anold Kayanda wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa wakati wa Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake, CSW69, jijini New York, Marekani.Mkutano huu muhimu kuhusu wanawake umefanyika kuanzia tarehe 10 hadi 21Machi 2025 na kuhudhuriwa na maelfu ya wanawake kutoka kote duniani naye Dkt. Rose Reuben akiwa mmoja wao.Kiongozi huyu wa waandishi wa habari nchini Tanzania anaona kwamba kuna hatua nyingi zimepigwa katika kipindi cha miaka 30 tangu kuwekwa kwa Azimio la Beijing ili kumkomboa mwanamke lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya.“Na hii kazi sipendi kujilaumu sana kwamba je, hakuna kitu ambacho kimefanyika?! Mambo yamefanyika mengi lakini masuala ya kijamii hayamaliziki kwa usiku mmoja kwasababu kila unapoamka jamii inabadilika kwa namna nyingine. Kwa hiyo tukitazama kwa mtazamo huo tunaona kwamba kuna kazi