Habari Za Un
24 MACHI 2025
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:12:15
- More information
Informações:
Synopsis
Hii leo jaridani tunaangazia hatari za usitishwaji wa misaada kutoka marekani kwa waathirika wa viruzi vya Ukimwi, na ujumbe wa washiriki wa Mkutano wa CSW69 uliokunja chamvi Ijumaa wiki jana. Mashinani tunakupeleka nchini Tanzania, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS leo limeonya kwamba kusitishwa kwa ufadhili wa Marekani sio tu janga kwa vita dhidi ya gonjwa hilo bali ni chachu ya vifo na ongezeko la maambukizi mapya. Flora Nducha amefuatilia onyo hilo lililotolewa leo mjini Geneva Uswisi na Mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS Winnie Byanyima alipozungumza na waandishi wa habari.Wakati Mkutano wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani ulioleta pamoja wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na mashirka yasiyo ya kiserikali(NGOs) ulikunja jamvi ijumaa tarehe 21 Machi wiki jana tulipata kuzungumza na wawakilishi wa Shirika lisilo la kiserikali la Forum for Women Democracy Development and Justice, FODAJ amba