Habari Za Un

29 APRILI 2025

Informações:

Synopsis

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika mkoa wa Mwanza kaskazini magharibi mwa Tanzania ambapo vijana wameshika hatamu kuboresha mustakabali wao. Pia tunakuletea muhtasari wa habari  na mashinani tunasalia hapa makao makuu.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kudumisha Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO, umeikaribisha kusainiwa kwa “Azimio la Kanuni” tarehe 25 Aprili 2025 mjini Washington, D.C chini ya usimamizi wa Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, kati ya serikali za DRC na Rwanda kwa lengo la kulinda rai ana kutekeleza azimio la Baraza la Usalama namba 2773 (2025).Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, Juliette Touma, akizungumza na waandishi wa habri mjini Geneva kwa njia ya video kutoka mji mkuu wa Jordan, Amman, wakati  kuzingirwa kwa Ukanda wa Gaza kukikaribia kuingia mwezi wa pili amesema “Mzingiro wa Gaza ni muuaji wa kimya muuaji wa watoto, wazee, na watu walioko katika mazingira magum