Habari Za Un

28 APRILI 2025

Informações:

Synopsis

Hii leo jaridani tunaangazia siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Kazini, na juhudi za Umoja wa Mataifa za kusaidia wakulima Sudan Kusini kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Makala tunasalia na usalama kazini na mashinani tunakwenda nchini Kenya, kulikoni?Leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Kazini mwaka huu ikibeba maudhui “Mapinduzi ya usalama na afya Kazini: Nafasi ya Akili mnemba na teknnolojia ya kidijitali mahala pa kazi” lengo likiwa kudhihirisha nguvu ya AI na teknolojia zinapotumika vyema zinaweza kuleta mabadiliko kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani ILO.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP nchini Sudan Kusini chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Korea KOICA wanaendesha mradi wa kusaidia wananchi katika kilimo ili kujenga ustahimilivu na kupambana na utapiamlo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Evarist Mapesa.Makala tunabisha hodi nchini Indonesia, taifa hili la Kusini-Mashariki mwa bara la Asia, kubwa hasa ni kumulika ni kwa vipi se