Habari Za Un

Kampuni Indonesia zachukua hatua kuimarisha usalama na afya pahala pa kazi

Informações:

Synopsis

Huko mashariki mwa Indonesia, kampuni za usindikaji samaki za PT Chen Woo Fisheries na PT Harta Samudra zimeongeza motisha wa kazi miongoni mwa wafanyakazi wake baada ya kuchukua hatua za kuimarisha usalama na afya pahala pa kazi. Hatua hizo ambazo zimeweka mazingira ya staha pahala pa kazi zinafuatia mradi wa pamoja wa shirika la Umoja wa Mataifa la kazi, ILO na Umoja wa Kampuni za Uvuvi na Usindikaji Samaki nchini Indonesia, AP2H1. Je nini kilifanyika na hali sasa iko vipi? Assumpta Massoi anafafanua zaidi katika makala hii inayoletwa leo hii ikiwa ni siku ya kimataifa ya usalama na afya pahala pa kazi.