Habari Za Un

25 APRILI 2025

Informações:

Synopsis

Hii leo jaridani tunaangazia wakimbizi wa DRC waliokimbilia Burundi, na ujumbe wa Siku ya Kimataifa ya Hakibunifu. Makala inatupeleka nchini Kenya kuangazia ugonjwa wa malaria na mashinani tunasalia hapa makao makuu katika mkutano wa Jukwaa la watu wa asili.Mazingira ya maisha kwa wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC waliongia Burundi na kupelekwa katika kambi ya wakimbizi ya Musenyi si endelevu na yanatishia mustakabali wao. Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR Ayaki Ito, amesema hayo leo huko Geneva, Uswisi wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu hali ya wakimbizi hao wanaoendelea kumiminika nchini Burundi.Kesho Aprili 26 ni Siku ya Kimataifa ya Hakibunifu - Siku ambayo ni fursa kwa ulimwengu kukumbushwa umuhimu wa haki kwa watu wanaobuni mambo mbalimbali duniani. Ili kufahamu zaidi kuhusu Hakibunifu tumezungumza na mtaalamu wa Sheria za Sanaa na Hakimiliki, Wakili Joshua Msambila wa nchini Tanzania, kwanza anaeleza kilichomsukuma yeye kujikita kati