Habari Za Un

15 MEI 2025

Informações:

Synopsis

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha katika mkutano wa CSW68 kumsikia Christina Kamili Ruhinda, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria nchini Tanzania, TANLAP. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno la wiki.Wakati dunia ikiadhimisha miaka 77 tangu Nakba ambapo zaidi ya wapalestina 700,000 walifurushwa kutoka vijiji na miji yao mwaka 1948, shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa Wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limetoa onyo kali kuhusu sura mpya ya mateso na ufurushwaji wa lazima uonaoendele Gaza.Akiwa na wasiwasi kutokana na ripoti za kuaminika kwamba wakimbizi wa Rohingya kutoka Myanmar walilazimishwa kushuka kutoka kwenye meli ya jeshi la wanamaji la India na kutoswa katika bahari ya Andaman wiki iliyopita, Mtaalamu wa UN wa Haki za Binadamu kuhusu wakimbizi wa Myanmar, ameanzisha uchunguzi kuhusu kitendo hicho alichoeleza kuwa ni cha kushangaza na kisichokubalika.Na baada ya muda mrefu kuonekana kama mchangiaji mkubwa wa uto