Habari Za Un

Bi. Joy :Teknolojia inatatua changamoto za kijamii - Wasichana katika TEHAMA

Informações:

Synopsis

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA, au ICT inaendelea kutawala na kuunda fursa mpya, lakini wanawake bado wanakumbana na changamoto kubwa ya upungufu wa uwakilishi. Hata hivyo, wanawake wanavuka mipaka na sasa Bi. Joy, msichana kutoka Nairobi Kenya, ambaye ni mtaalamu katika teknolojia ya kidijitali, amekalia nafasi muhimu katika kubadili mtindo wa maisha kupitia elimu ya ICT. Katika mahojiano na washirika wetu Radio Domus, alizungumzia umuhimu wa kuhamasisha wasichana kujiunga na masomo ya teknolojia ili kutengeneza mustakabali mpya wa kidijitali, na kubadili dunia kwa njia ya kidigitali na usawa. Sharon Jebichii na Makala zaidi