Habari Za Un

19 MEI 2025

Informações:

Synopsis

Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya afya, na wakimbizi wa Syria wanaorejea nchini mwao. Makala tukwenda nchini Kenya kumulika ufukaji wa nyuki, na mashinani tunakuletea ujumbe wa Katibu Mkuu wa IMO kuhusu Siku ya Kimataifa ya wanawake mabaharia.Wajumbe kutoka kote duniani wamekusanyika mjini Geneva, Uswisi, kwa ajili ya Mkutano wa 78 wa Baraza la Afya Duniani (WHA78) unaofanyika kuanzia leo Mei 19 hadi 27 Mei mwaka huu.Tangu kuangushwa kwa utawala wa aliyekuwa Rais wa Syria Bashar al Assad aliyekuwa madarakani kwa zaidi ya muongo mmoja, wananchi wa Syria wamekuwa wakimiminika kurejea nchini mwao ambapo takwimu za sasa zinaonesha zaidi ya Wasyria 500,000 wamerejea kutoka nchi jirani. Mmoja wa waliorejea ni Babu Jassim na Leah Mushi anatuletea simulizi yake.Katika makala tunaelekea Kajiado nchini Kenya, ambako juhudi za utunzaji mazingira kupitia mradi wa ufugaji wa nyuki unaofadhiliwa na shirika la misaada la Marekani USAID kwa kushirikiana na idara ya misitu ya Kenya KFS hazichangii tu katika kukuza uchum