Siha Njema

Matatizo ya tezi ya koo ambayo yanaweza kukusababishia matatizo ya akili

Informações:

Synopsis

 Matatizo ya tezi ya koo ,kwa kawaida  yananaletwa na upungufu au wingi wa madini aina ya iodine ambayo huzalishwa na tezi (thyroid gland).  Homoni inapokuwa kidogo hali ambayo inafahamika kama Hypothyroidism, hii inaashiria kwamba tezi inafanya juhudi za hali ya juu kutafuta madini hayo .Mtu aliye na hali hii ,anakuwa hana nguvu ,nywele kudondoka  na hata mzunguko wake wa mwezi wa damu huvurugika.Madini hayo yanapokuwa mengi inamanisha tezi inafanya kazi kupitliza kuzalisha homoni iliyozidi  kwenye mzunguko wa damu na kuchanganyika na vitu vingene ambavyo husababisha kutengeneza kama sumu fulani ambayo huchoma mafuta yaliyo kwenye hifadhi mwilini, mishipa ya fahamu huathirika kiasi kidogo.Mtu ambaye ameathiriwa na aina hii ya pili, huanza kupunga uzito na umbo la mwili taratibu baadaye madhara yanapoongezeka mtu anaanza kupoteza kumbukumbu, anakuwa na hasira, anakula sana, nywele zinanyonyoka mpaka anapata upara, magoti yanakosa nguvu na mtu anashindwa kutembea.Moyo kwenda mbio , macho yanavimba sehemu ya ju