Synopsis
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.
Episodes
-
Kauli ya rais wa Tanzania Samia Suluhu kuwazuia wanaharakati wa nchi zingine
20/05/2025 Duration: 09minLeo tunaangazia ,hatua ya Tanzania kuwazuia Mawakili, wanaharakati wa haki za binadamu kutoka nchini Kenya, akiwemo Jaji Mkuu mstaafu Willy Mutunga waliokwenda kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi mkuu wa upinzani Tundu Lissu. Rais Samia Suluhu Hassan, amesema serikali yake haitaruhusu wanaharakati wa kigeni kuingia nchini Tanzania na kuingilia masuala ya ndani ya nchi yake.
-
Nini kifanyike kumaliza vita vinavyoendelea Sudan,Ukraine na Gaza
19/05/2025 Duration: 10minViongozi wa dunia, wameendelea kutoa wito wa amani kwenye nchi za Sudan Ukraine na Gaza hizo, ambako vita vimesababisha vifo vya maelfu ya raia na wengine kuwa wakimbizi. Hata hivyo licha ya wito huu, mapigano yameendelea kuripotiwa.
-
-
Maoni ya waskilizaji kuhusu vipindi vyetu juma hili
09/05/2025 Duration: 09minJuma hili waskilizaji wetu walikuwa na maoni haya kuhusu taarifa zetu
-
Je kuna hofu ya kutokea kwa vita vya tatu vya dunia
08/05/2025 Duration: 10minKatika makala haya tunajadili athari ya vita vya ukraine na Urusi na sasa tishio la vita nyingine kati ya India na Pakistan. Je ni shara ya kutokea kwa vita vya pili vya dunia ? ndilo swali tumekuuliza. Skiza baadhi ya maoni ya waskilizaji.
-
News Zealand kudhibiti mitandao ya kijamii kwa watoto
07/05/2025 Duration: 09minShaba ya makala haya inalenga news Zealand ambapo serikali inapendekeza marufuku ya matumizi ya mitandao kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 16, lengo likiwa kuwakinga dhidi ya athari za mitandao. Njia gani wazazi wa kiafrika wanaweza kuwalinda watoto na mitandao ya kijamii? Ndilo swali tumeuuliza na haya hapa baadhi ya maoni yako, skiza makala haya.
-
Dunia uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari
05/05/2025 Duration: 09minLeo mada yetu inajikita kwa siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari, ambapo Umoja wa Mataifa umesema licha ya baadhi ya nchi kupiga hatua katika ulinzi wa wanahabari, hofu ya uhuru wa habari kuendelea kuminywa inaendelea kutanda. Mwaka jana jumla ya wanahabari 82 walipoteza maisha wakitekeleza majukumu yao. Tuambie nchini mwako vyombo vya habari viko huru? Haya hapa baadhi ya maoni yako, skiza makala.
-
-
-
Mchakato wa kumchagua kiongozi mpya wa kanisa katoliki duniani
28/04/2025 Duration: 10minKwa sasa macho yakiwamulika makadinali 135 watakaochagua papa mpya ndani ya siku chache zijazo, mjadala kuhusu Papa kutoka Afrika ukishamiri.Mchakato wa kumchagua p
-
Joseph Kabila adaiwa kurejea DRC kupitia Goma
21/04/2025 Duration: 09minJuma lililopita ripoti ambazo hazijathibitishwa rasmi zilieleza kuwa rais wa zamani wa DRC, Joseph Kabila alirejea nchini Mwake kupitia mji wa Goma unaokaliwa na waasi wa M23 wanaosaidiwa na Rwanda. Hata hivyo hatua yake imeifanya serikali ya Kinshasa, kusimamisha shughuli zote za chama chake cha PPRD, ikikituhumu kushurikiana na waasi hao.Unazungumziaje kurejea kwa rais Kabila?Ndilo swali tumekuuliza katika makala haya.Skiza maoni ya mskilizaji.
-
DRC: Kujerea kwa Joseph Kabila kwaibua hisia mseto
10/04/2025 Duration: 10minKatika makala haya shaba yetu inalenga nchini DRC, ambapo Rais mustaafu wa DRC, Joseph Kabila, ametangaza kurejea nchini humo, kutoka nchini Afrika Kusini ambako amekuwa akiishi kwa zaidi ya mwaka moja , ili kuchangia kutafuta suluhu kwa mzozo wa usalama mashariki mwa nchi yake. Unazungumziaje hatua hii ya Kabila? Ndilo swali tulikuuliza, skiza makala haya kuskia maoni ya waskilizaji wetu.
-
Marekani : Rais Donamd Trump atangaza ushuru zaidi kwa bidhaa za kigeni
09/04/2025 Duration: 10minKwenye makala haya tunajadili, hatua ya rais wa Marekani, Donald Trump kutangaza kuongeza ushuru kwa bidhaa zote zanazoingizwa Marekani, kutoka mataifa ya Kigeni, hatua inayoonekana kutikisa uchumi wa Dunia. Je unahisi hatua ya rais Trump ni sahihi?Ndilo swali tumeuuliza.Skiza makala haya kujua maoni ya waskilizaji.
-
Kenya: Yawarejesha nyumbani raia wake waliotapeliwa kuenda Mynamar
08/04/2025 Duration: 09minShaba yetu kwenye makala haya inalenga hatua ya Serikali ya Kenya, kueeendelea kuwarejesha mamia ya raia wake waliotapeliwa na kusafirishwa hadi nchini Myanmar kwa ahadi ya kupewa ajira. Nchini mwako visa kama hivi vinaripotiwa?Ndilo swali letu, skiza makala haya kuskia baadhi ya maoni ya waskilizaji.
-
Africa Mashariki : Viongozi watathimini kudhibiti mitandao ya kijamii
08/04/2025 Duration: 09minKatika makala haya tunajadili haja ya kuwepo sheria za kudhibiti mitandao ya kijamii kwa baadhi ya mataifa ya Africa Mashariki. Skiza makala haya kuskia mano ya waskilizaji wetu.
-
Maoni ya waskilizaji kuhusu wizi unaofanywa kwenye mizani na wafanyabiashara
05/04/2025 Duration: 10minMakala haya ni maoni ya waskilizaji kuhusu ripoti maalum ya namna wananchi wanavyopigwa na wafanyabiashara kwenye mizani wanapopimiwa nafaka mbalimbali za chakula, huku gesi ya kupikia pia ikitajwa.
-
-
DRC: Majadiliano ya kitaifa kuhusu kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa kitaifa
25/03/2025 Duration: 10min -
Qatar : Yakutanisha Kagame na Tshisekedi
20/03/2025 Duration: 09minShaba yetu leo kwenye makala haya inalenga taifa la Qatar ambapo taifa hilo juma hili lilifanikiwa kuwaleta pamoja marais Felix Tshiesekedi wa DRC na mwenzake wa Rwanda Paul Kagme, katika juhudi za kutafuta suluhu kwa mzozo wa mashariki ya DRC. Unafikiri Qatar itafanikiwa kuzima mzozo wa mashariki mwa DRC. Skiza makala haya kujua baadhi ya maoni ya waskilizaji.
-
Kenya : Kanisa katoliki latangaza marufuku kwa wanasiasa
19/03/2025 Duration: 10minTunajadili hatua ya Kanisa la Anglikana nchini Kenya, kwa mara nyingine limesisitiza marufuku ya kuwazuia wanasiasa kuzungumza kanisani katika juhudi za kuzuia wanasiasa kufanya siasa kanisani. Je unazungumziaje hatua hii ya kanisa Anglikana nchini Kenya? Skiza makala haya kuskia baadhi ya maoni ya waskilizaji wetu.