Synopsis
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episodes
-
Tanzania: UNICEF na Ubalozi wa Uholanzi wamesaidia kupunguza magonjwa Kilolo
28/03/2025 Duration: 01min -
-
28 MACHI 2025
28/03/2025 Duration: 09minUmoja wa Mataifa watuma salamu za rambirambi kufuatia tetemeko barani Asia.UNICEF na Ubalozi wa Uholanzi wamesaidia kupunguza magonjwa Kilolo, Tanzania.Makala ni kuhusu Siku ya Kimataifa ya Kutozalisha Taka.Mashinani tunamulika ubunifu wa Janet Chemitei wa Tengeneza Cafe katika urejelezaji nguo nchini Kenya.
-
METHALI: NDOTO NJEMA HAIHADITHIWI
27/03/2025 Duration: 01minKaribu kujifunza Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani na anafafanua methali Ndoto njema haihadithiwi.
-
27 MACHI 2025
27/03/2025 Duration: 11minKaribu kusikiliza jarida la Umoja wa Mataifa ambapo hii leo tunaendelea na kuwasikia wadau waliohudhuria mkutano uliomalizika wiki iliyopita wa Kamisheni ya hali ya wanawake CSW69 unaotathmini Azimio la Beijing na Mpango wa Utekelezaji vilivyopitishwa mwaka 1995 katika mkutano wa 4 wa kimataifa wa wanawake huko Beijing China. Pia utapata fursa ya kusikiliza muhtasari wa habari na kujifunza kiswahili ambapo leo utapata ufafanuzi wa methali "NDOTO NJEMA HAIHADITHIWI"
-
Chad: Wanakikundi watumia faida ya biashara yao kuanzisha shule
26/03/2025 Duration: 03minNchini Chad, wanawake wanakikundi cha kutengeneza sabuni na mafuta ya kupata mwilini wameamua kuchukua hatua ili umamuma wa kutokujua kusoma na kuandika ambao umewakumba wao, usiwakumbe pia watoto wao wa kike. Wanakikundi hao wa APROFiCA wanaopata ufadhili kutoka Benki ya Dunia wameona ni vema kuchukua hatua hiyo ili kufanikisha lengo namba 4 la Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs la Umoja wa Mataifa kuhusu elimu, kwani elimu ni mkombozi kwa binadamu. Je wamefanya nini? Assumpta Massoi anafafanua kupitia video ya Benki ya Dunia.
-
UN: Hali inazidi kuwa tete Gaza huku watu zaidi ya milioni wakiwa hatarini kukosa mlo
26/03/2025 Duration: 02minWatu zaidi ya milioni 1 wako katika hatari ya kukosa chakula endapo misaada haitoruhusiwa kuingia Gaza wakati huu mashambulizi makali ya Israel yakizidisha janga la kibinadamu yameonya leo mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa. Flora Nducha na taarifa zaidi.
-
-
Baada ya kukimbilia Burundi, wakimbizi wa DRC wakubwa na uhaba wa mahitaji muhimu
26/03/2025 Duration: 02minHali ya kibinadamu ya wakimbizi zaidi ya 100,000 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, waliokimbilia nchini Burundi kusaka usalama kutokana na mapigano mashariki mwa nchi yao katika katika kipindi cha chini ya miezi mitatu, iliyopita ni ya mashaka, wakati huu ambapo ufadhili unazidi kukumbwa na mkwamo, wakikabiliwa na uhaba wa huduma kama chakula, huku kukiwa na pengo la ufadhili. Je ni madhila yapi? Sharon Jebichii anafafanua zaidi kupitia video iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR.
-
25 MACHI 2025
25/03/2025 Duration: 11minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo tunasalia hapa makao makuu katika mkutano wa CSW69 uliokunja chamvi Ijumaa wiki jana, tunamsikia aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa 4 wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake, Mkutano wa Beijing Bi. Gertrude Mongella.Hapa New York, Umoja wa Mataifa leo umetoa wito wa kuachiliwa kwa wafanyakazi wake wanaoshikiliwa kote ulimwenguni ambao wamejikuta matatani wakati wakiwahudumia watu walio katika hatari, huku wakihatarisha usalama wao binafsi kwa kukabiliwa na vitisho vya kutekwa nyara, vurugu, unyanyasaji, na kifungo katika maeneo yenye migogoro na majanga.Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kuhusu vifo vya watoto imeonya kwamba miongo ya maendeleo katika kupunguza vifo vya watoto na watoto wachanga wakati wa kuzaliwa yako hatarini kutokana na kupunguzwa kwa ufadhili. Idadi ya vifo vya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano ilipungua hadi watoto milioni 4.8 mwaka 2023, huku vifo vya wakati wa kuzaliwa vikiendelea kubaki
-
Wanawake wamefanya mengi lakini hayajarekodiwa - Dkt. Reuben CSW69
24/03/2025 Duration: 03minRekodi ni chache sana ya vitu ambavyo wanawake wamefanya hapa duniani, anasema Dkt. Rose Reuben, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania anapozungumza na Anold Kayanda wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa wakati wa Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake, CSW69, jijini New York, Marekani.Mkutano huu muhimu kuhusu wanawake umefanyika kuanzia tarehe 10 hadi 21Machi 2025 na kuhudhuriwa na maelfu ya wanawake kutoka kote duniani naye Dkt. Rose Reuben akiwa mmoja wao.Kiongozi huyu wa waandishi wa habari nchini Tanzania anaona kwamba kuna hatua nyingi zimepigwa katika kipindi cha miaka 30 tangu kuwekwa kwa Azimio la Beijing ili kumkomboa mwanamke lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya.“Na hii kazi sipendi kujilaumu sana kwamba je, hakuna kitu ambacho kimefanyika?! Mambo yamefanyika mengi lakini masuala ya kijamii hayamaliziki kwa usiku mmoja kwasababu kila unapoamka jamii inabadilika kwa namna nyingine. Kwa hiyo tukitazama kwa mtazamo huo tunaona kwamba kuna kazi
-
UNAIDS: Kusitishwa kwa ufadhili wa Marekani ni janga kubwa kwa vita dhidi ya ukimwi na chachu ya vifo
24/03/2025 Duration: 02minShirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS leo limeonya kwamba kusitishwa kwa ufadhili wa Marekani sio tu janga kwa vita dhidi ya gonjwa hilo bali ni chachu ya vifo na ongezeko la maambukizi mapya. Flora Nducha amefuatilia onyo hilo lililotolewa leo mjini Geneva Uswisi na Mkurugenzi mtendaji wa UNAUDS Winnie Byanyima alipozungumza na waandishi wa habari.
-
24 MACHI 2025
24/03/2025 Duration: 12minHii leo jaridani tunaangazia hatari za usitishwaji wa misaada kutoka marekani kwa waathirika wa viruzi vya Ukimwi, na ujumbe wa washiriki wa Mkutano wa CSW69 uliokunja chamvi Ijumaa wiki jana. Mashinani tunakupeleka nchini Tanzania, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS leo limeonya kwamba kusitishwa kwa ufadhili wa Marekani sio tu janga kwa vita dhidi ya gonjwa hilo bali ni chachu ya vifo na ongezeko la maambukizi mapya. Flora Nducha amefuatilia onyo hilo lililotolewa leo mjini Geneva Uswisi na Mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS Winnie Byanyima alipozungumza na waandishi wa habari.Wakati Mkutano wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani ulioleta pamoja wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na mashirka yasiyo ya kiserikali(NGOs) ulikunja jamvi ijumaa tarehe 21 Machi wiki jana tulipata kuzungumza na wawakilishi wa Shirika lisilo la kiserikali la Forum for Women Democracy Development and Justice, FODAJ amba
-
FODAJ CSW69: Vita dhidi ya dhulma kwa wanawake na wasichana
24/03/2025 Duration: 02minWakati Mkutano wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani ulioleta pamoja wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na mashirka yasiyo ya kiserikali(NGOs) ulikunja jamvi ijumaa tarehe 21 Machi wiki jana tulipata kuzungumza na wawakilishi wa Shirika lisilo la kiserikali la Forum for Women Democracy Development and Justice, FODAJ ambalo linasaidia wasichana na wanawake waathirika wa ukatili wa kijinsia katika kaunti ya Kajiado nchini Kenya. Sharon Jeichii anaeleza waliochokizungumzia.
-
Zanzibar tumetekeleza kwa vitendo azimio la Beijing: Waziri Riziki Pembe
21/03/2025 Duration: 05minWakati mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW69 ukifikia ukingoni mshiriki kutoka Zanzibar Tanzania ameweleza Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili kwamba Zanzibar imepiga hatua kubwa katika usawa wa kijinsia na utekelezaji kwa vitendo matakwa ya Azimio la Beijing la usawa wa kijinsia na hatua. Je wametekeleza vipi na hatua gani walizopiga? Ungana nao katika mahojiano haya.
-
Ukiwekeza kiuchumi kwa mwanamke basi umewekeza katika jamii: Janet Mbene mshiriki CSW69
21/03/2025 Duration: 05minMkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani CSW69 unakunja jamvi leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani baada ya mjadala wa wiki mbili kutathimini hatua zilizopigwa na changamoto zilizosalia miaka 30 baada ya azimio la Beijing la usawa wa kijinsia nah atua za utekelezaji. Flora Nducha amebahatika kuzungumza na mmoja wa wakishiri wa mkutano huo kutoka asasi za kiraia nchini Tanzania
-
IFAD yawaepusha vijana wa kike 5 na kazi za ndani na kuwajengea stadi za kilimo biashara Senegal
21/03/2025 Duration: 02minTukiwa bado ndani ya mwezi wa Machi, unaotambuliwa kuwa ni mwezi wa wanawake tunakwenda nchini Senegal ambako huko wasichana waliokuwa wakifanya kazi za ndani, wamewezeshwa na Umoja wa Mataifa na sasa ni wakulima na wanatumia stadi za upigaji na utengenezaji video za mtandaoni kuelimisha jamii kuhusu kilimo chenye tija. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
-
21 MACHI 2025
21/03/2025 Duration: 10minHii leo jaridani tunaangazia mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW69 unafikia tamati hii leo Machi 21 hapa katika makao makuu, na wakulima wanawake nchini Senegal. Mashinani inatupeleka nchini Tanzania kumulika mradi wa maji.Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW69 unafikia tamati hii leo Machi 21 hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Bi. Gertrude Mongella, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa 4 wa Kimataifa wa wanawake maarufu kama Mkutano wa Beijing uliofanyika mnamo mwaka 1995, hivi tunavyozungumza, pamoja na umri wake mkubwa ameshirikia karibia vikao vyote vya mkutano huu wa CSW69 ambao pia ulikuwa unaangazia utekelezaji wa maazimio yaliyowekwa miaka 30 iliyopita chini yake mama Mongella.Tukiwa bado ndani ya mwezi wa Machi, unaotambuliwa kuwa ni mwezi wa wanawake tunakwenda nchini Senegal ambako huko wasichana waliokuwa wakifanya kazi za ndani, wamewezeshwa na Umoja wa Mataifa na sasa ni wakulima na wanatumia stadi za upigaji na ut
-
Wanaume 'wapenzi wetu' msiwe na hofu na sisi - Bi. Gertrude Mongella
21/03/2025 Duration: 01minMkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW69 unafikia tamati hii leo Machi 21 hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.Bi. Gertrude Mongella, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa 4 wa Kimataifa wa wanawake maarufu kama Mkutano wa Beijing uliofanyika mnamo mwaka 1995, hivi tunavyozungumza, pamoja na umri wake mkubwa ameshirikia karibia vikao vyote vya mkutano huu wa CSW69 ambao pia ulikuwa unaangazia utekelezaji wa maazimio yaliyowekwa miaka 30 iliyopita chini yake mama Mongella.Nilipokutana naye nimemuuliza swali hili la kichokozi.Mazungumzo zaidi kati yangu na Mama Gertrude Mongella yatakujia katika vipindi vyetu vijavyo hivi karibuni.
-
Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa maneno "Ashiraf, Janabi, gayagaya, kiti cha marimba na kiti cha msaji"
20/03/2025 Duration: 59sKatika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno “Ashiraf, Janabi, gayagaya, kiti cha marimba na kiti cha msaji”